Ligi Kuu

Mbrazil avunja rekodi ya Coastal Union

Sambaza....

Ile rekodi nzuri kabisa ilikua inashikiliwa na “Wagosi wa Kaya” Coastal Union chini ya mwalimu Juma Mgunda imefikishwa kikomo na kiungo Mbrazil wa Simba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Coastal Union kabla ya mchezo wa leo walikua wamepata ushindi katika michezo mitano mfululizo  waliyokua wamecheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani.

Gerson Fraga akishangilia baada ya kufunga goli.

Mabao mawili ya kiungo Mbrazil wa Simba Gerson Fraga katika kila kipindi cha mchezo yameifanya Simba kupata ushindi na kunyakua alama zote tatu mbele ya Wagosi wa Kaya.  Kwa matokeo hayo sasa Coastal Union wanabaki nafasi ya tatu wakiwa na alama zao 30 huku Simba wakiendelea kubaki kileleni wakiwa na alama 47.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Taifa kwa kiasi kikubwa eneo la kuchezea lilitawaliwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea jijini Dar es salaam na hivyo kupunguza ladha ya Kandanda. Huku wachezaji wa timu zote mbili  wakioenekana kuteseka na hali ya uwanja.

Gerson Fraga akifunga goli lake la kwanza kwa kichwa.

Goli la kwanza la Simba lilitokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Cleotus Chama na kufikia Fraga akiwa peke yake hivyo kupiga kichwa kwa utulivu na kumuacha kipa wa Coastal hoi. Goli la pili lilitokana na shuti kali la Hassan Dilunga kumshinda kipa wa Coastal na kujikuta akiutemea uwanjani na kumkuta Fraga akiwa katika eneo zuri la kumalizia mpira huo na kuukwamisha wavuni.

 

Sambaza....