Ligi Kuu

Tuwekeze kwenye soka la vijana zaidi..

Sambaza....

Endelea kusoma sehemu hii ya sita ya mfululizo wa makala ya ‘Mh. Mwakyembe, Winners take control’

Ligi kuu ya soka nchini Congo DR Linafoot inaweza kuwa ni ligi isiyotajwa sana lakini ni miongoni mwa ligi inayokusanya wachezaji wengi wa kigeni kutoka nchi za afrika ya kati, Mashariki, Magharibi na hata Kusini mwa jangwa la sahara huku vinara wakiwa ni TP Mazembe FC kutoka Mbuyi mayi nakati ya Lubumbashi mitaa ya Kamarondo chini ya Rais wake Moise Chapwe Katumbi, lakini lini ulisikia wakisema wageni wanazuia vipaji vyao? Ama umewashi kusikia lini wakilalamikia kushindwa kwa timu yao ya taifa kama ni sehemu ya wachezaji wageni waliopo TP Mazembe ama AS Vita Club au hata Darling Club Motema Pembe ama FC Eloi Lupopo?

Pamoja na kukusanya wachezaji wa kigeni Congo DR timu yao ya ktaifa imeendelea kupata nafasi ya ushiriki wa kudumu kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa Barani Afrika na hata kuwa timu mojawapo inayopigania nafsi za kufuzu kombe la Dunia mara kwa mara; sababu ni moja wana timu imara sana na vilabu imara sana na wachezaji imara sana, wakati Heritier Ebenezer Makambo hana nafasi kwenye ligi ya Congo ya kupata kuwapo tu kwenye vilabu viwili vikubwa vya AS Vita na TP Mazembe achana na kuitwa timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo Jean Mac Mundele Makusu aliyekuwa mshambulizi hatari sana wa AS Vita Club akiendelea kuiota alitoka kuja Tanzania na kuwa bidhaa ghali sokoni; Itoshe tu kusema kama Makusu hana nafasi kwenye Timu ya taifa ya Congo wanaopata nafasi wakoje? Ndipo utakapopata majibu ukitajiwa majina ya wachezaji kama Cedric Bakambu, Yannick Bolasie, Benik Afobe na Dieumerci Mbokani na wengine wengi wanaocheza soka barani ulaya.

Waziri wa Michezo Dr. Harrison Mwakyembe kipekee tu niseme shida ya timu yetu ya taifa kufanya vibaya, na hata wachezaji wetu kutokuwa bora hakusababishwi na wachezaji 40 ama 50 wa kigeni waliopo kwenye ligi yetu kati ya wachezaji wote 600 wa vilabu 20 vya ligi kuu, shida ipo kubwa sana, nafahamu wewe ni Mbobezi kwenye masuala ya Tafiti, ombi langu kwako niseme tu badala ya kuja na njia hii ya kutafuta majibu ya mkato basi tafiti zifanywe, tupate kujua tatizo ili tu tulitibu tatizo hilo na sio kuishia kupambana na viashiria tu; niseme kama uwepo wa wachezaji wa kigeni ni tatizo kwa vijana wetu basi haitakuwa zaidi ya asilimia 0.2 tu mengineyo ni matatizo yetu ya msingi.

Kotei (Kushoto) akimthibiti Muleka wa TP Mazembe

Rejea kwa majibu ya Robin van Persie kwa kijana wake Shaqueel WINNERS TAKE CONTROL, vipi wachezaji wetu wa kitanzania wangapi waliacha shule wakisema eti sababu walipenda zaidi mpira? Je uko mtaani kuna walimu/ makocha wangapi wenye sifa stahiki za kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto wetu ikiwa hawa tunaotegemea waje kuwa makocha waliacha shule darasa la nne ama la saba ama hawakufanya mitihani ya kidato cha nne; ilhali Kozi za Ualimu wa mpira wa miguu za kuanzia Leseni C ya CAF shirikisho la mpira barani Afrika linataka walau Mshiriki wa Kozi hiyo awe na elimu ya Kidato cha nne!

Tigana Lukinja (Mtangazaji wa East Africa Radio) alipokuwa nchini Ghana katika cliniki ya watoto.

Tufukuze wageni sawa lakini je kuna ijtihada gani za dhati zimefanywa katika kuweka miundo mbinu, nyenzo na hata mazingira ya kulea na kukuza watoto wetu kuja kuwa wachezaji warithi wa akina Luis Miquissone tutakao wafukuza leo? Makampuni mangapi ama Mashirika mangapi ya Kiserekali ama Kiraia ambayo yako tayari kuweka pesa zake kwenye mashindano ya watoto ambayo FIFA wanakazia kuwalea watoto kushindana na sio kuwapa tamaa ya kushinda makombe bila kufika umri sahihi? Kama nchi jambo lipi kubwa endelevu tumeliwekea kipaumbele ukiachana na zile mbio zetu za kuandaa mashindano ya vijana wa chini ya miaka 17 mwaka 2019? Ikowapi Falsafa ya nchi kuhusu Soka la Nchi hii? Mwaka juzi wakati tukipata mafanikio ya timu zetu za vijana kwa kuwekeza kidogo kwa ile TFF ya akina Jamal Malinzi toka  mwaka 2013 ikowapi dira ya Taifa baada ya yale mashindani kuisha?

Simba Sports Club mwaka mmoja uliopita ilifanikiwa kucheza hatua ya robo fainali ya mashindano ya Vilabu Bingwa  barani Afrika asilimia 60 hadi 70 ya wachezaji waliokuwa wakianza muda wote wa mechi za mashindano yale na katika kulithibitisha hilo katika mechi dhidi ya Al Ahly kwenye uwanja wa Taifa mechi ambayo Simba SC ilishinda kwa goli moja kwa sifuri Ilianzisha wachezaji watatu tu wazawa ambao ni Aishi Manula, Jonas Mkude na John Bocco huku wachezaji nane wakiwa ni wageni ambao walikuwa mabeki Zana Coulibaly na Pascal Wawa (Ivory Coast) Asante Kwasi (Ghana), Juuko Mursheed (Uganda) Viungo James Kotei (Ghana) naClatous Chama (Zambia), Washambuliaji Meddie Kagere (Rwanda) na Emmanuel Okwi (Uganda), huku wengine wawili wakiwa kwenye benchi wakisubiri Haruna Niyonzima (Rwanda), Nicholas Gyan (Ghana) sasa wakati huu tunasema wageni wanabana nafasi ya wazawa tupige picha wachezaji wazawa halafu tulinganishe uwezo wao na uwezo wa wachezaji wa khariba ya Okwi, Kagere, Chama, Benard Morison, Yakoub Mohammed, Haruna Niyonzima  na wengine wenye uwezo wa juu sana ambao wameendelea kuifanya Ligi yetu kuwa bidhaa takikana  sokoni.

Haruna Niyonzima akipiga mpira mbele ya nahodha wa Simba Mohamed Hussein

Washabiki wa mpira, wachambuzi wa mpira hata hawa tuliowapa dhamana ya kuongoza mpira wote wana mawazo sawa; kwa kuwa tu wote wanaishi miongoni mwao na siku zote matokeo ya mpira ya kushangaza yakitokea utasikiwa wakisema That’s Football”kwamba ni matokeo yaliyotokea kwa bahati; nakubali kwamba bahati ipo lakini mpira hautavuka mstari wa lango bila kufanyika kwa vitu vingi vyenye uhusiano chanya, unaona timu kama Simba Sports Club kwa miaka mitatu sasa wamekuwa na nguvu sana wakishinda karibia mechi zao zote vivyo hivyo Yanga Sports Club walishinda karibia mechi zao zote miaka 4 ama 5 iliyopita unataka kujua sababu ni nini?


Soma mfululizo wake sehemu ya 7 na ya mwisho..

Jadili na Mwandishi wa makala hii katika sehemu ya maoni….

Sambaza....