Aishi Manula mlinda mlango wa Simba ambae mashabiki wanamlaumu kwa kuwarudisha Yanga mchezo kwa kuruhusu magoli ya kizembe
Ligi Kuu

Wachezaji wa Kigeni Hawaviui Vipaji vyetu..

Sambaza....

Hii ni sehemu ya mwisho ya makala yetu ya ‘Mh. Mwakyembe, Winners take control

Basi moja ya sababu hizo itakuwa Mishahara; ndio ni Mishahara kwasababu kama tutaamua kuchambua kwanini mishahara huku tukiegemea kwenye timu inayoshinda mfululizo basi tutafahamu hili; timu inayoshinda walau kila mchezo ni kwamba wanalipa mishahara mikubwa ama mishahara mizuri kwa wachezaji wao; basi kama hoja ni mishahara na vivyo hivyo watakuwa wana wachezaji wazuri zaidi waliopo sokoni na hapa ndio nataka kusimika mzizi kwamba wachezaji wa kigeni sio hoja ya msingi ya kufeli kwa wachezaji wetu wachezaji wetu wanapaswa kuongeza viwango vyao na kuwa bora ili wasajiliwe na timu zinazotaka kuwa bora na kupata matokeo bora vinginevyo ni kuvionea tu hivi vilabu kwa kuweka Kanuni kandamizi kwao. Ni sawa tu na mtu wa kawaida aliyeamua kwenda kununua bidhaa nje ya nchi, moja ya sababu zake atakwambia ameenda kununua nje kwasababu ndani hakuna bidhaa bora kulinganisha na hiyo aliyoifata nje kwenye soko la ndani.

Karia, Rais wa TFF

Vivyo hivyo na kwenye soka pia; kama unataka timu ya ubingwa ama timu ambayo kila mwaka inakupa nafasi ya kuwania ubingwa, basi unapaswa kufanya kazi endelevu katika kujenga timu ambayo itakuingizia Mapato kila mwaka, mapato ambayo yatakufanya usajili wachezaji bora na wenye talanta waliopo soko la ndani na nje, wachezaji ambao watakufanya ushindanie mataji kila msimu kwa kupigana kwa machozi, jasho na damu huku ukiwa na Viongozi bora ambao wataendelea kuitenda kazi yao vizuri kwa kulipa mishahara kwa wakati, kuweka mazingira rafiki kwa wadhamini, washika dau na hata wateja (mashabiki) na hili haliendani hata kidogo na bahati.

Sasa kuwaondosha hao wachezaji ina maana waliowekeza pesa zao kwenye mpira ambazo ni mapato kwa Vilabu vyetu waziondoe pesa zao kwasababu hakuna mdhamini atataka kuweka kwenye timu itakayoshindwa kumhakikishia ushindi mara kwa mara kwa kutumia “simple logic tu kushindwa kwa timu ndio kushindwa kwa bidhaa” hivyo basi kama timu itakuwa na wachezaji wasio bora kisa ni wazawa tu basi itapoteza mvuto wake kwa wadhamini, lakini pia itapoteza uwezo wake kushindana ndani ya uwanja kwa mechi za ndani na hata za kimataifa; vivyo hivyo ndio itakapoelekea kupoteza mvuto wake hata kwa wachezaji mahiri aambao walivutika kwasababu timu ilifanya vizuri kimataifa kwa hizo nafasi 5 au chache mtakazoona zinafaa kwenye kanuni mpya.

Mwandishi wa Makala hizi. Bofya picha kuzipata makala zaidi.

Hapa ndipo Robin van Persie alipomwambia mwanae “If you want to be a loser? Be a loser and if you want to be a winner take control of your life and stop complaining about others” wachezaji wetu kama ndio wanamtazamo huu basi waache kulalamika mara moja na wapiganie maisha yao ya soka la sivyo wakubali tu kuwa losers potelea mbali kwasababu wao wameamua kuwa wacheza mpira kwa mapenzi yao wenyewe kwa kuamua kuacha shule kisa tu waliupenda sana mpira hivyo wawe tayari kupigania kitu walichokipenda na sio kuanza kubebwa bebwa tu kiholela holela; Mimi kama mshabiki na muandishi wa Makala hii siko tayari kuwa sehemu ya timu yenye wachezaji wa hovyo, ama wenye kiwango hafifu, nitaendelea kuwa na tabia ile ile ya Mteja mwenye uhitaji wa bidhaa bora sokoni.

Ushauri wangu wa pekee kwa TFF na Mamlaka husika kwenye hili la wachezaji wa kigeni ni kuweka kanuni ambazo zitazilazimisha Vilabu kuleta wachezaji wa kutoka nje wenye uwezo mkubwa zaidi ama wenye kitu cha ziada ambacho ndani ya nchi wachezaji wetu wamekosa hivi ndivyo nchi zote zilizoendelea wamefanya huwezi kwenda kucheza ligi kuu Uingereza, Hispania, Ujerumani ama Ufaransa achilia mbali hizi ligi za daraja la kati za Uberege ama Ufinishi, kiwango bora kikiambatana na vitu vya ziada visivyopatikana kwa wachezaji wazawa vitakufanya ucheze huko kwao; sio Lazima tuwaige Misri ama Morocco ama nchi zozote za ukanda huo kwamba wao wameweka ukomo hivyo basi nasi lazima tuweke; tujiulize kwanza yanapokuja mashindano makubwa ya Afrika ama ya Dunia wachezaji wangapi wanaotoka kwenye ligi za ndani za nchi hizo wanafanikiwa kujumuishwa kwenye vikosi vyao vya timu za Taifa vinavyoanza mechi?

Mh. Mwakyembe (Kulia)

Kwa sasa tuachane na hii dhana kwamba wachezaji wageni wanaua vipaji vya wazawa tujikite kwenye kuboresha miundo mbinu, kuboresha mitaala ya soka, kutengezea falsafa ya mpira wetu kuanzia kwa watoto wa miaka 15 hadi timu ya wakubwa huku tukiwaelimisha watoto wetu kwamba mpira unachezwa kwa akili ili tuvune wachezaji na wasomi pia ambao baada ya kumaliza mpira wao tupate makocha na wakufunzi wenye weledi na wenye elimu ya kutosha kufuatia watoto wetu wengi kuchagua mpira wakisema niliacha shule kwasababu ya mpira leo hii Makocha kutoka nchi jirani ndio wanaofundisha Vilabu vya ligi kuu hii ni ishara tosha kwamba hata huku chini kwenye chanzo cha hawa wachezaji hakuna walimu kabisa na kama wapo basi hawana ubora wa kutosha kulea na kuendeleza watoto wetu, muda sasa umefikakuachana na hili suala la ukomo wa namba ya wachezaji wa kigeni ambao wamekuja kubadilisha taswira ya soka letu kimataifa na hapo ndipo tutawafanya watoto wetu walioacha shule sababu ya mpira wapiganie kitu walichokipenda zaidi ya Elimu!

Otherwise we can decide to be a loser as WINNERS TAKE CONTROL of their Lives and never complain about OTHERS!

©️Mdidi the Writer 😎


Soma mfululizo wa makala zilizopita pia…..

Jadili na Mwandishi wa makala hii katika sehemu ya maoni….


Sambaza....