Feisal Salum akisalimiana na Jonas Mkude katika mchezo dhidi ya Simba
Ligi Kuu

Mkude anachakujifunza kwa Feisal Salum “Toto”

Sambaza....

Jonas Gerald Mkude alifunga goli maridhawa sana akiwa uwanja wa Taifa katika mchezo wa Ligi ya Mabinga Afrika dhidi ya Nkana Rangers ya Zambia. Alipiga shuti kali la umbali wa Mita 25 na kufanikiwa kuisawazishia Simba iliyokua imetanguliwa bao moja na Nkana.

Hakuna ubishi kua Jonas Mkude ni kiungo bora wa kati kwa sasa hapa nchini mbele ya kina Mudathir Yahya, Sure Boy (Azam fc), Feisal Salum (Yanga), Jumamme El Fadhil (Prisons) Mtenje Albano (Coastal Union) Hassan Dilunga Kenny Ally (Singida utd) na wengine wengi.

Pengine msimu huu chini ya kocha Patrick Ausems amezidi kua mtamu baada ya kubadilishiwa majukumu na kusogezwa mbele huku chini yake akiwa James Kotei. Kwa kupata uhuru huu wakucheza Mkude amezidi kua mchezaji muhimu ndani ya uwanja.
Uwezo mkubwa wa kuchezesha timu n kukaba hilo halipingiki kwa Mkude lakini amekua na tatizo moja ambalo anaweza kuiga mbele ya Mpemba Feisal Salum na kuzidi kua mkamilifu katika eneo la kiungo.

Jonas Mkude amekua akikosa uwezo na shabaha ya kufunga magoli ya mbali. Mkude amekua sio mthubutu wa kupiga langoni akiwa Mita 20 mpaka 30 ambapo kiutaalamu ndio aina ya magoli ambayo viungo wanatakiwa wafunge.
Jonas Mkude anatakiwa amwangalie Feisal Salum “Fei toto” jinsi ambavyo anaweza kufunga akiwa kwenye eneo la kiungo kwa mipira iliyokufa ama kwa “re-bound” kama alivyofanya katika michezo kati ya KMC na Ruvu Shooting.
Si Feisal tuu hata “swaiba” wake Said Hamis Ndemla “daktari” anaweza kua darasa tosha katika upigaji wa mashuti ya mbali.

Baada ya kufunga goli lile zuri dhidi ya Nkana huenda ikapita tena miaka mingi ndipo aje kufunga goli zuri kama lile kama ambavyo imepita miaka mitano alipowafunga Tanzania Prisons goli kama hili uwanja wa Taifa.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x