Feisal Salum akisalimiana na Jonas Mkude katika mchezo dhidi ya Simba
ASFC

Mkude tayari kuifwata Yanga!

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa robo fainali wa kombe la FA kati ya Azam fc na Simba sc, klabu ya Simba imepata nafuu katika eneo la kiungo baada ya Jonas Mkude kumaliza adhabi yake na kupona majeraha aliyoyapata katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC.
Lakini pia kocha mkuu wa Simba Sven ameongeza kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao lakini yeye na benchi lake la ufundi wamekiandaa kikosi kwa ajili ya ushindi na ana matumaini ya kuhakikisha  Simba inavuka kwenda  nusu fainali ambapo itakutana na Watani zao Yanga sc.
Sven Vandebroeck
Sven “Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, tunajua Azam ni timu imara, ingawa tumeifunga katika mechi tatu zote zilizopita lakini bado haitufanyi tujisikie itakuwa rahisi tumejipanga kuhakikisha tunashinda.”
Pia kiungo Jonas Mkude amemaliza adhabu yake ya kutumikia mechi mbili alizokuwa amefungiwa na atakuwa huru kucheza kama benchi la ufundi litaona inafaa.
Kocha Sven amekuwa akiwatumia Said Ndemla, Gerson Fraga na Mzamiru Yassin katika eneo analocheza Mkude ingawa kwenye mechi ya leo huenda akaanzishwa.
David Molinga na Mrisho Ngassa wakishangilia goli katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar.
Mshindi wa mchezo wa leo atakwenda kukutana na Yanga sc ambao jana walifanikiwa kuwafunga Kagera Sugar katika mchezo wa robo fainali uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini la Dar es salaam.

Sambaza....