Uhamisho

Mo: Simba haikusajili vizuri.

Sambaza....

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Mohamed Dewji “Mo” amekiri mfumo walioutumia msimu uliopita kufanya usajili haukua mzuri kabisa ndomana baadhi wa wachezaji walifeli kuitumikia Simba ipasavyo katika msimu uliomalizika.

Mo amekiri hayo alipokua akiongea na Waandishi wa habari, na kusema njia walizotumia kuwapata wachezaji hao hazikua sahihi kabisa hivyo watabadili mfumo wa kupata wachezaji wapya ili kuitumikia klabu ya Simba.

“Hatuna mfumo mzuri wa “scouting lazima nikiri hilo, msimu uliopita tulikosea. Unaona tuliwapata Wabrazil watatu lakini mpaka sasa amebaki mmoja tu.

Mlinzi wa Simba Tairone Santos akipambana na Ditram Nchimbi wa Yanga.

Mwaka jana tulitumia kampuni ya kutoka Afrika Kusini lakini walituangusha sana.” Mohamed Dewji.

Mo pia amegusia katika  uwekezaji wa vijana na kusema wanategemea kuanza na timu za vijana za U14, U17 na U20 ambao wakaa pamoja.

Mohamed Dewji “Kwa kuanzia tutakua na timu tatu za vijana tutafanya, angalau kila timu iwe na wachezaji 25. Tutafanya scouting nchi nzima tunataka hata mtoto wa maskini aje kuichezea Simba.

Hatutawapangia mitaani, watakaa hostel pamoja wajifunze falsafa ya Simba wakue katika misingi ya Simba.”

 

Sambaza....