Feisal Salum akisalimiana na Jonas Mkude katika mchezo dhidi ya Simba
Ligi Kuu

Morrison na Mkude kumbe lao moja na TFF!

Sambaza....

Wachezaji wawili nyota wa Simba na Yanga leo wamepokea hukumu zao kutoka Shirikisho la soka nchini TFF kutoka katika kamati ya nidhamu ya wachezaji.

Kiungo Jonas Mkude wa Simba na Benard Morrison wamehukumiwa kukosa michezo miwili ya Ligi pamoja na faini ya shilingi laki tano kila mmoja.

Benard Morisson.

Benard Morrison amepata adhabu hiyo baada ya kumpiga kiwiko “kipepsi” Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Jonas Mkude na yeye pia alifanya kitendo kama hicho baada ya kumpiga kiwiko Ally Kombo Biashara United katika mchezo ambao Simba waliibuka ushindi wa bao tatu kwa moja katika uwanja wa Taifa


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.