Sambaza....

Mshambuliaji wa zamani wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid, aliekosa nafasi katika klabu yake ya sasa ya Simba Sc amepata nafuu baada ya klabu mbalimbali za Ligi Kuu Bara kuonyesha nia ya kumuhitaji kwa mkopo.

Mohamed Rashid ameonekana kua lulu kwa baadhi ya vilabu wakitaka huduma yake huku baadhi ya vilabu vikipeleka barua rasmi kwa klabu yake ya Simba kumuomba kwa mkopo.

Vilabu vya KMC, Mwadui, Allience na klabu yake ya zamani ya Tanzânia Prisons ni baadhi ya klabu zinazotaka huduma ya Mo Rashid.

Klabu ya Simba Sc kwa upande wao wameridhia mchezaji wao kuondoka ili apate nafasi ya kucheza mara kwa mara na hivyo ni kazi kwake kuchagua klabu ya kwenda!

Sambaza....