Simon Msuva mfungaji wa bao pekee dhidi ya Uganda katika mchezo wa ugenini
Tetesi

Msuva Kutua Simba, Yanga Kutambulisha Chuma Kipya Junamosi Kwenye Mkutano Mkuu

Sambaza....

Mmshambuliaji Simon Msuva ameziingiza vitani klabu tatu kubwa Simba,Yanga, Azam kuwania saini yake baada ya kumaliza mkataba na timu ya Al Qadisiyah FC ya Saudi Arabia na sasa vigogo hao watauana. (Mwanaspoti)

Imebainika kuwa, kuna chuma kipya Yanga kipo mjini tayari na huenda kikatambulishwa kupitia mkutano mkuu wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Jumamosi katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Sport Xtra)

Rasmi Klabu ya Simba imeachana na nyota wake wa muda mrefu Jonas Gerald Mkude, Simba walitoa taarifa hiyo jana kupitia ukurasa wake wa instagram.

Feisal Salum akisalimiana na Jonas Mkude katika mchezo dhidi ya Simba. Nyota wote wawili hao hawatokua na timu zao hizo msimu ujao.

Simba pia imetangaza kuachana na Benno Kakolanya na Erasto Nyoni ambao wanaungana na nyota wengine walioachwa Simba kina Nelson Okwa, Victor Akpan, Augustine Okrah na Mouhamed Outtara.

Singida Fountaine Gate na Simba wapo katika mpambano wa kumuwania kiungo wa Mbeya City Hassan Maulid Machezo. Mkataba wa Machezo unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Mwanaspoti)

Kocha wa zamani wa Mamelody Sundowns Pitso Mosimane na kocha mpya wa Al Wahda ya Falme za Kiarabu (UAE), amesema Nasreddine Nabi ana vigezo vyote kuwa kocha wa Kaizer Chiefs. (Kick offs)

Pitso Mosimane (kushoto) akiwa na viongozi wa Yanga na GSM Injinia Hersi Said na Ghalib.

Mlinda mlango na nahodha wa Al Ahly amesema walitamani kukutana na Mamelody Sundows katika hatua ya fainali na sio Wydad Casablanca waliowafunga na kutwaa ubingwa wa klabu bingwa Afrika. (King foot)

Mshambulizi wa Liverpool Mohamed Salah, 31, ndiye mchezaji mwingine anayesakwa na Saudi Pro League baada ya kuwasili kwa Karim Benzema na N’Golo Kante. (Four Four Two)

Borussia Dortmund wanapanga kutoa kitita cha pauni milioni 13 kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Tunisia Hannibal Mejbri, 20, ambaye msimu uliopita alichezea Birmingham kwa mkopo . (Manchester Evening News)

Sambaza....