Mabingwa Ulaya

Mzimu wa Bernabeu unavyowatafuna wapinzani wa Madrid!

Sambaza....

Kama umepata kuusikia uwanja maarufu Santiago Bernabeu “machinjioni” hukujua kwanini unaitwa hivyo basi nikupe sababu

Santiago Bernabeu ni jina la mshambuliaji nyota wa zamani wa klabu hiyo aliyecheza kwa vipindi viwili tofauti na kuwafanyia makubwa sana Madrid akiwa na wastani wa mechi moja bao moja nadhani hapo unapata picha alikuwa mshambuliaji wa aina gani

Alizaliwa Mwaka 1895 kwa wazazi Jose Bernabeu Ibeneza Nunez na Mama Antonio de Yeste ambayo kwa tamaduni za wenzetu kuna kuwa na muunganiko wa majina kutoka koo ya Baba na Mama.

Santiago Yeste Bernabeu.

Ndiyo maana mwanaume huyu aliitwa Santiago Bernabeu Yeste hivyo basi ukitaka kuutamka uwanja huo ni lazima uutamke kwa majina matatu ili kuleta maana.

Kikawaida tunafahamu kuna viwanja vingi vina majina ya watu au hata mitaa lazima uwe umelifanyia jambo timu au jamii husika ndiyo wakutunuku heshima ya eneo lao kutumika kama utambukisho.

Sasa basi kwa minajiri hiyo uwanja ulistahili kuitwa jina hilo kwa mchango wake moja kwa moja kabla ya kuja kuongoza tena klabu kwa akiwa Rais kwa miaka 35 nadhani ndiyo rekodi ya kiongozi wa juu aliyekaa muda mrefu ( 1943-1978) ambapo alifariki akiwa madarakani.

Santiago Yeste Bernabeu.

Tukimuangalia kwenye wakati wake wa kuwa mchezaji kama nilivyotangulia kusema wastani wake wa kufunga ilikuwa 1:1 maana yake alikuwa anauwezo wa kucheza michezo 20 /20 hii scoring ability ni ya hali ya juu mno.

Kwa mafanikio haya ya Real Madrid msimu huu kupata nafasi ya kucheza fainal dhidi ya Liverpool May 28 2022 Stade de France kumechagizwa na ‘jinamizi ‘lake.

Karim Benzema akishangilia goli dhidi ya PSG.

Real baada ya kumaliza vinara kwenye makundi, hatua ngumu ya mtoano walikutana na PSG ambapo kwenye mchezo wa kwanza walipoteza bao 1 la jioni kabisa, lakini walivyofika Santiago Bernabeu Yeste wakakubali kichapo cha 3-1 na kutupwa nje.

Hatua ya robo fainali wakakutana na Chelsea ambapo walishinda Stanford Bridge 3-1 upepo ukawa mbaya nyumbani kwao Santiago Bernabeu Yeste wakapoteza 3-2 lakini goli la pili la Madrid lilikuja toka wapi na kwa muda gani? muda muafaka au la! Utakubaliana nami jinamizi la Santiago liliendelea kuwatafuna wageni huku likileta neema kwa wenyeji.

Karim Benzema akishangilia mbele ya mlinda mlango wa Chelsea Eduardo Mendy.

Nusu fainali pia kama jana kama juzi wakati Kocha Joseph Pep Guardiola akianza kutengeneza pattern ya kucheza fainali na Liverpool ghafla mleta magoli yake Santiago      (jinamizi) likaleta magoli mawili ya haraka na kuipeleka kwenye dakika zaa nyongeza.

Ambapo hakuwaacha wapweke alikumbuka mjukuu wake mpendwa ambaye ndiyo mrithi hajatikisa nyavu akamletea goli la mazingira ya penati. 

Rodrygo akishangilia goli la pili alilowafunga Manchester City.

Hapa ndiyo machinjioni Santiago Bernabeu Yeste hatoki mtu, uwanja pekee unakupa uhakika wa goli hivyo ni juhudi zako tu kulipachika.

Tukutake 28/05/22 uwanja wa Taifa wa Ufaransa


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.