Sambaza....

Kiungo matata wa Simba sc Said Hamis Ndemla “Daktari” anaiacha klabu yake ya Simba iliyo katika michezo muhimu ya Klabu Bimgwa Africa na kuelekea Ulaya ili kutimiza ndoto zake za kucheza soka nje ya Tanzania.

Said Ndemla anaondoka leo usiku kuelekea Ulaya akiwa na wakala wake. Na alipotafutwa mratibu wa klabu ya soka ya Simba alithibitisha hilo na kuweka wazi kua anaiacha Simba na kutimkia zake Ulaya japo hakuweka wazi ni klabu gani wala nchi gani anaelekea.

“Ndemla anaondoka leo usiku kuelekea Kwenda Ulaya, alikuja kuniaga na nimempa ruhusa hiyo hivyo leo jioni hatutakua nae katika mazoezi.” Mratibu wa Simba Abbas Ally alithibitisha. Pia aliongeza “Sijui anakwenda klabu gani, ni wakala wake ndie anaejua Ndemla anakwenda klabu gani na kufanya nini. Sijajua kama anakwenda kusaini mkataba au ni kwaajili ya majaribio”

Kwa taarifa zilizopo inasemekana Ndemla anakwenda katika klabu ya Afc Askistuna ya nchini Sweden ambapo alifuzu majaribio kabla ya kurudi tena nchini kusaini mkataba na Simba mwanzoni mwa msimu huu. Lakini klabu hiyo imemuomba kimuangalia tena kama bado yupo timamu kabla ya kumpa mkataba.

Sambaza....