Uhamisho

Ni Wakati wa Neema, Hofu na Majuto kwa Wachezaji.

Sambaza....

Wapwa, tunaelekea mwisho wa ligi ya NBC na maandalizi ya usajili kwa baadhi ya vilabu yashaanza. Ni kipindi chenye sura tofauti kwa mchezaji neema/hofu na majuto ndani yake.

Makocha ambao wanauhakika wa kuendelea na timu zao wao wanaaendelea na usajili wa msimu ujao kimya kimya kama ‘kumnyatia mwenye ulemavu wa kusikia’.

Mara nyingi mchezaji anapocheza ndani ya msimu huwa anakuwa na malengo ya kujipambanua ili auzike kwenye timu zenye machungio bora zaidi, kwa maana ya malisho mema yakifedha.

Mlinzi wa Simba Mohamed Hussein akitafuta mbinu za kimthibiti mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele, wawili hao wamekua wakitajwa kuhitajika na vilabu vya Afrika Kusini.

Lakini ikishindikana hivyo upambane uwe na uhakika wa kubakia timuni mwako yaani ikiwezekana uwe umecheza juu ya nusu mechi za msimu kama NBC maana yake 15.

Na ikiwa tofauti kama umri wako ni mdogo angalau uwe umecheza robo ya mechi za msimu yaani mechi saba mpaka nane hivi, wanaweza kukuvumilia kwa ajili ya msimu ujao au kukupeleka kwa mkopo kama unamkataba mrefu kwa ajili ya kupandisha kiwango na kupata muda zaidi wa kucheza.

Wapo wale manguli ambao hawana hofu na lolote ana namba ya kudumu ndani ya timu amejiamini na kuaminika ana uhakika wa kuwepo yeye anachowaza ni dau kuongezeka tu kila msimu.

Kelvin Kongwe Sabato miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu na Ligi Kuu wakiwa katika harakati za usajili kila msimu unapomalizika.


Kazi kwenu wachezaji kama ukiitumikia timu kwa ufasaha wewe unauhakika kama si kuuzwa basi kubakia kwenye timu yako msimu ndiyo huoo unaisha kama vinginevyo nawe sawa tu.

Sambaza....