Tetesi

Pep athibitisha nyota wake anaondoka!

Sambaza....

Pep Guardiola amethibitisha Leroy Sane ataondoka Manchester City msimu huu wa joto baada ya mazungumzo yasiyokuwa na matunda juu ya kuongezwa kwa mkataba.

Bosi huyo wa Man City alithibitisha kwamba kilabu hicho kilitaka kuendelea kua na nyota huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 24, ambaye amekuwa akihusishwa sana na Bayern Munich, lakini  nyota huyo amekiri anataka kutafuta changamoto mpya.

Leroy Sane

Pep Guardiola “Leroy alisema hataki kuongeza mkataba wake. Ikiwa anataka kuondoka na itafanyika msimu huu wa joto au mwisho wa mkataba. Klabu iliongea nami mara kadhaa, alikataa mkataba wake hivyo anataka kucheza katika kilabu kingine.

Nadhani kila mtu anajua na ikiwa mwishoni mwa msimu huu makubaliano yanaweza kupatikana ataondoka, ikiwa sivyo ataondoka mwishoni mwa mkataba wake.”


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.