Uhamisho

Rashid Juma wa Simba mikononi mwa Polisi

Sambaza....

Kiungo mshambuliaji wa pembeni wa Simba sc Rashid Juma amefanikiwa kujiunga na timu ya Polisi Tanzania kwa mkopo akitokea Simba katika usajili huu unaoelekea mwishoni.

Rashid Juma amejiunga na Polisi Tanzania kwa mkopo wa mwaka mmoja akikimbia Msimbazi kutokana na ufinyu wa nafasi ya kucheza mbele ya kina Luis Miquissone, Francis Kahata na Hassan Dilunga lakini pia maingizo mapya kina Charles Ilanfia, Benard Morrison na Cris Mugalu.

Rashid Juma akitambulishwa katika klabu ya Polisi Tanzania

Rashid Juma ni zao la Simba B ambapo alifanya vizuri akiwa chini ya Mwalim Mussa Hassan Mgosi na kupelekea kupandishwa kikosi cha wakubwa kilichokua chini ya Patrick Auseems.

Akiwa Polisi atakwenda kuungana na Ramadhani Pires, Daruesh Saliboko pamoja na Shabani Haruna kwenda kuunda safu mpya ya ushambuliaji.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.