Sambaza....

Kuna vitu vingi wamevifanya, kuna rekodi nyingi wameziweka , rekodi ambazo zimewafanya wawe na mashabiki wengi duniani.

Lakini kuna baadhi ya rekodi hawajawahi kuzivunja au kuzifikia na zinaonekana ni ngumu kwao kuzifikia hasa hasa kwenye michuano ya klabu bingwa barani ulaya.

Juzi Ronaldo alifunga hat-trick yake ya 50 na kumuacha Messi kwa Hat-hatricks 8 akiwa na hat-hatricks 42, pamoja na kwamba wana hat-tricks nyingi lakini wote hawajaifikia rekodi ya Bafetimbi Gomis aliyefunga Hat-trick ya haraka zaidi, alitumia dakika nane (8) kufunga hat-trick hiyo.

Bafetimbi Gomis

Wote wawili wameshacheza fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya lakini hawajafikia rekodi ya kufunga magoli mengi katika fainali moja ya UEFA iliyowekwa na Ferenc Puskas aliyefunga magoli 4 kwenye fainali moja.

Messi na Ronaldo kwa pamoja wameshafikisha umri wa miaka 30, umri ambao mtu akifikia inaonekana kama ndiyo mwisho wake wa maisha ya soka. Paolo Maldini alifunga goli kwenye fainali ya UEFA akiwa na umri wa miaka 36 , Francesco Totti ashawahi kufunga goli kwenye michuano ya UEFA akiwa na umri wa miaka 38, hivo basi Messi na Ronaldo wanadaiwa kuvunja au kufikia rekodi ya kufunga goli kwenye michuano ya UEFA wakiwa na umri mkubwa.

Paolo Maldini

Wote wawili washawahi kuwa wafungaji bora katika mashindano hii Klabu ya bingwa lakini hawajawahi kuifikia rekodi ya Radamel Falcao aliyewahi kufunga magoli 18 ndani ya msimu mmoja akiwa FC Porto.

Pamoja na uwezo wao wa kufunga lakini hawajawahi kuvunja rekodi ya kufunga goli la mapema katika michuano ya ƙklabu bingwa barani ulaya inayoshikiliwa na Roy Makaay aliyefunga goli ndani ya sekunde 10

Sambaza....