Ligi Kuu

Sabato huyu wa Kagera hana tofauti na Håland wa Dortmund

Sambaza....

Tukiwa tupo kwenye mapumziko ya soka kwa asilimia kubwa duniani baada ya janga la Corona kuchachamaa. Mwenzangu kwa uangalifa kutoka kitengo cha Tunzo, Thomas Mselemu, alimtembelea Kelvin Sabato nyumbani kwake Tabata kwaajili ya kumkabidhi zawadi zake wakati mtandao wetu ukisheherekea naye kwa kupachika mabao matano mwezi Februari.

Sabato ameshaifungia Kagera Sugar mabao saba toka ajiunge nao katika usajili wa dirisha dogo, hivyo basi binafsi nilijaribu kuangazia kwa undani zaidi usajili bora wa dirisha dogo nikaona kuna wachezaji watatu kwenye ligi kuu Tanzania bara VPL ambao usajili wao umeleta tija kwa haraka zaidi.

Mosi ni Kelvin Sabato Kongwe akitokea Gwambina FC kwenda Kagera sugar, Pili ni Bernard Morrison akitokea Orland Pirate kwenda Yanga na tatu ni Deogratius Motisha ‘Dida’ usajili huru baada ya kuachwa Simba Sc alipojiunga na Lipuli FC. Dida pamoja kwamba yeye ni golikipa, usajili wake umekidhi mahitaji yao kama timu, imepata kipa atakayeweza kuzuia magoli ikiwemo kuanzisha mashambulizi. Pia ni golikipa pekee mwenye goli moja msimu huu wa 2019/20, akiwa amefunga goli hilo katika open game (Sio la penati).

Kevin Sabato akiwa na zawadi zake baada ya kuibuka Galacha wa mabao kwa mwezi Februari

Lakini kubwa kuliko yote ni uwezo mkubwa aliouonyesha Kelvin Sabato, Galacha wa Magoli wa Kandanda mwezi Februari, kwa muda mchache tangu ajiunge na Kagera dirisha dogo. Amefunga magoli sita (6) VPL. Hakika magoli haya ni mengi mno, hata huenda ikawa kwenye level za akina Erling Braut Håland, raia wa Norway anayecheza wa Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Swali la kujiuliza ni kwanini bwana mdogo huyu katakata kwa haraka?. Mfumo ambao Kocha wa Kagera sugar, Mecky Mexime anautumia ni 4-3-3 ambao unampa nafasi mshambuliaji wa aina hii kuweza kushine kwa sababu unaruhusu kukimbia eneo kubwa uwanjani kusaka mipira. Maana by natura huyu ni fighter na yupo makini kwenye tendo la kufunga (finisher au goal poacher) mzuri huku akisaidiwa kwa ukaribu na akina Yusuph Muhili (Magoli 10), Zawadi Mauya, Kapama Uweso, Mwalyanzi Siseme na wengineo.

Pamoja na kijiunga na Kagera dirisha dogo bado alikuwa na nafasi ya pili ya kucheza Namungo Fc yenye maskani yake Mjini Lindi, timu ambayo alipohojiwa na mtandao huu alikiri ndiko ambako angekuwa kama si Kagera Sugar.

Tukumbuke Sabato ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa na Ligi Kuu tangu anacheza Majimaji (aliuambia mtandao huu hapo ndipo alipofunga bao zuri zaidi dhidi ya Mbeya City) kisha Mtibwa na hatimaye kujiporomosha yeye binafsi toka ligi kuu hadi ligi daraja la kwanza kule Gwambina Fc (Timu pekee yenye uwanja wa hadhi yake Tanzania).

Image result for gwambina fc

Kwa haraka kama angechanga karata zake vyema kisha kuamua kwenda kule Namungo yumkini asinge fanikiwa kwa kiwango alichonacho sasa.

Kwanini? Mosi ni aina ya kocha ambaye angeenda kufanya naye ni raia wa kigeni. Yumkini akawa anafahamiana naye kwa mara ya kwanza hivyo pressure ingekuwa kubwa kutaka kucheza na kutimiza maagizo ya mwalimu wake, tofauti na alivyo chini ya Mecky ambaye alishafahamiana ikiwemo kufanya kazi pamoja kabla. Pia, Kocha Thierry Hitimana ni kama ana kikosi fulani cha kudumu katika timu yake na wachezaji wake wa safu ya ushambuliaji wote wamewaka (wako vizuri), Reliant Lisajo (Magoli 11 ), Blaise Bigirimana (Magoli 9), George Makanga (Magoli mawili), Nzigamasabo Styve na kiungo mchezeshaji Lukas kikoti (Magoli manne) na kiungo wa pembeni mwenye balaaa zake Hashimu Manyanya (Tazama hapa).

Naangalia quality (ubora) ya wale wasiopata nafasi Mara kwa Mara viwango vyao kama Hamisi Halifa, Mohammed Ibrahimu (Mo) aliyetoka Simba Sc hivyo nakwenda kuamini kuwa kwenda kwake Namungo ingekuwa karata mbaya (bad card) na kinyume chake kwa Kagera ingekuwa rahisi zaidi. Kama ambayo imekuwa sasa, urahisi wake ni kutokana na kucheza Mtibwa sugar ambayo ni pacha wa Kagera kwa maana ya kushabihiana kwa vitu vingi ndani ya timu.

Mwisho ni kumpogeza mchezaji mwenyewe kwa super performance yake, na utayari wake kama alivyosema wakati akiongea na mtandao wetu kuwa yupo tayari kupambana kuisaidia Kagera Sugar inafanya vizuri.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.