Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi leo wanaingia mzigoni tena katika muendelezo wa Sportpesa super cup dhidi ya AFC Leopard ya Kenya, lakini itawakosa nyota wake muhimu kuelekea robo fainali hiyo

Simba sc na Mbao ya Mwanza ndio wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya Sportpesa baada ya wawakilishi wengine wa Tanzania timu za Yanga na Singida United kutolewa.

Kuelekea mchezo wa kesho Simba sc leo ilifanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Bokko Beach huku ikiwakosa baadhi ya nyota wake muhimu kutokana na sababu mbalimbali.

Erasto Nyoni (katikati) atakosa michuano yote Sportpesa baada kuumia goti.

Katika mchezo wa kesho Simba itawakosa John Bocco, Erasto Nyoni walio majeruhi, pia wamo majeruhi wa muda mrefu Salim Mbonde na Shomari Kapombe. Wachezaji wote hao hawakuwepo katika mazoezi ya mwisho leo asubuhi.

Pia Simba sc itamkosa beki wake Asante Kwassi ambae hayupo nchini akiwa amerejea kwao nchini Ghana. Said Ndemla atakosekana pia ambae yupo nchini Sweden kwenye majaribio.

Sambaza....