Ligi Kuu

Simba: Ruvu Shooting hawaiwezi vita!

Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Simba tayari ameanza kutuma salamu kwa Ruvu Shooting kuelekea mchezo wao wa NBC Premier League utakaopigwa Jumapili hii saa moja kamili usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ahmed Ally akizungumza na kituo cha redio amesema siku zote Ruvu ni watu wa kutangaza vita lakini vita hawaviwezi.

Kibu Denis wa Simba akipiga mpira mbele ya Rashid Juma wa Ruvu Shooting

“Sina hakika kama wameshafika Dar es salaam ama kwao Mlandizi kwasababu walikua mbali kidogo (Kigoma).

Kuna kutangaza vita na kupigana vita miaka yote Ruvu huwa wanatangaza vita lakini huwa hawana uwezo wa kupigana vita.,” Ahmed Ally

Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba

Msemaji huyo wa klabu ya Simba pia hakusita kuonyesha dhamira yao ya kutaka alama tatu katika mchezo huo na akijinasibu kuibuka ba ushindi kama ambavyo walifanya katika mchezo wa raundi ya kwanza.

“Mnyama anaingia katika mchezo wa Jumapili kutaka ushindi na si kingine chochote.
Wajiandae (Ruvu Shooting) pakubwa wanakutana na Mnyama ambae mechi tatu hajapata ushindi. Kile ambacho kilimtokea CCM Kirumba atapata kipigo zaidi ya hapo.” Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.