ASFC

Simba ya Lwanga na Benno kuelekea kisasi cha msimu!

Sambaza....

Simba na Yanga wanakwenda kukutana mara ya nne msimu huu katika nusu fainali ya kombe la FA katika dimba la CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Wababe hao walikutana katika mchezo wa Ngao ya Hisani katika mchezo wa kufungua Ligi na Yanga kuibuka na ushindi wa bao moja la Fiston Mayelle.

Walipokutana tena katika michezo yote miwili ya Ligi iliisha kwa suluhu na hivyo kuifanya kuendelea kuwa mbabe wa Simba katika msimu kwa kumfunga mara moja na kupata suluhu mbili.

Beno Kakolanya akinyaka mpira katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El-Merreck.

Hivyo kuelekea mchezo wa nusu fainali ya FA ni wazi Simba atakua na kisasi cha kulipa kwa Yanga ili “ku-level scorebody”.

Kuelekea kisasi hicho ni kama Simba imeanza kupungiwa na silaha zake muhimu baada ya kuachana na Benard Morrison lakini pia majeruhi ya Aishi Manula na Jonas Mkude ni kama yanawapunguza nguvu Simba.

Sikiliza hapa jinsi Simba itavyojaribu kuziba pengo la Jonas Mkude na Aishi Manula kwa kuwatumia kina Benno Kakolanya na Thadeo Lwanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.