Wekundu wa msimbazi Simba sc leo ilikua na mkutano na waandishi wa habari na kuelezea kuhusu mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Africa dhidi ya Nkana ya Zambia.
Ikumbukwe Simba ilipoteza mchezo wake wa kwanza jijini Kitwe kwa mabao mawili kwa moja na hivyo kutegemea mchezo wa marudiano ili kupata ushindi na kufuzu hatua ya makundi
Kuelekea mchezo huo Simba imetangaza viingilio vya mchezo huo utakaopigwa December 23 Jumapili. Viingilio hivyo vitakua:
VIP A : Tshs20,000, VIP B: Tshs10,000 Mzunguko Tshs 3,000.
Katika hatua nyingine msemaji wa timu hiyo Hajji Manara amewahimiza Wanasimba wajae uwanjani na kufika kwa wingi uwanja wa Taifa. Manara ” Wanasimba na Watanzania kwa ujumla mje kwa wingi uwanja wa Taifa, mje kuisapoti Simba ili iweze kufuzu katika makundi baada ya miaka 13.” Manara ameongeza “Tujitahidi tuujaze uwanja kama inavyokuaga siku ya Simba Day hakika hata wale wa upande wa pili watakaokuja kuisapoti Nkana tutawazidi kwa kelele zetu”
Aidha Manara pia amepanga kukutana na vikundi vyote vya ushangiliaji na uhamasishaji vya Simba siku ya Alhamisi ili kuweka mikakati kabambe ya ushangiliaji siku ya mchezo.