Sven Vandebroek na Selemani Matola
ASFC

Sven: Dumayo anatakiwa achukuliwe hatua stahiki.

Sambaza....

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Sven Vandebroeck ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha Frank Dumayo kumuumiza mlinzi wake wa kulia Shomary Kapombe katika mchezo wa ASFC dhidi ya Azam fc.

Akizungumzia mchezo mbaya  aliyofanyiwa  Shomari Kapombe na Frank Dumayo kocha Sven amesema lilikuwa tukio baya na anaamini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litachukua hatua stahiki.

Shomari Kapombe akiwa amebebwa kutolewa nje ya uwanja baada ya kuchezewa madhambi na Frank Dumayo.

“Kama mchezaji wetu Jonas Mkude alifungiwa mechi mbili kwa kufanya madhambi basi naamini hata kwa aliyemfanyia Kapombe naye atachukuliwa hatua stahiki,” amesema kocha Sven alipokua akiongea na tovuti rasmi ya Simba.

Kapombe aliumizwa goti la mguu wa kulia kiungo Frank Domayo dakika za mwisho za mchezo tukio ambalo mwamuzi hakuliona.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.