Kombe la Dunia

Tanzania kuwajua wapinzani wake leo!

Sambaza....

Kuelekea kombe la Dunia litakalofanyika mwaka 2022 nchini Qatar tayari harakati za kufuzu michuano hiyo kwa nchi wanachama wa FIFA zimeanza kushika kasi huku Tanzania tukiwa wamoja wapo tunaotafuta nafasi hiyo adhimu.

Baada ya kufanikiwa kuwaondosha Burundi katika hatua ya awali sasa Tanzania inasubiri upangwaji wa makundi ili kuweza kuanza safari ya kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Kikosi cha Taifa Stars katika mchezo dhidi ya Burundi!

Leo saa mbili usiku makundi yatapangwa ili kujua Tanzania itakua katika kundi gani, kila kundi litashirikisha timu 4 huku kinara wa kila kundi ndie atakaepata nafasi ya kusonga mbele.

Makundi yatakua kumi yanayoshirikisha nchi nne katika kila kundi, kila kinara wa kundi atakwenda kucheza Playoff na vinara wengine ili kupata timu tano zitakazoiwakilisha Africa nchini Qatar.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.