Rais wa TFF Wallace Karia
Blog

TFF ipo “busy” haitaki mchezo na timu za Taifa.

Sambaza kwa marafiki....

Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF mwaka huu ni kama mwaka wao kutokana na ratiba ya CAF na FIFA kuwabana  haswa.
Unaweza sema TFF chini ya Rais Wallace Karia inakiona cha moto kutokana na kutakiwa kuhakikisha timu zote za Taifa zinaenda sawasawa kwenye mstari kuanzia maandilizi kwa maana ya kambi mpaka kupata ushindi.

TFF ndie msimamiaji mkuu wa masuala yote ya mpira wa miguu hapa nchini  hivyo ni wao wanapaswa kuzihudumia na kuzisimamia timu  zote za Taifa.

Tovuti yako ta Kandanda.co.tz tumekuwekea hapa baadhi ya matukio na mechi ambazo zipo ndani ya kalenda ya msimu wa mwaka 2018/2019 kwa timu za Taifa.

Taifa Stars vs Uganda

Tarehe 24 March Taifa Stars ilifanikiwa kuandika historia ya kufuzu Afcon kwa mara ya pili baada ya kuifunga Uganda mabao matatu kwa sifuri. TFF kwa kushirikiana na serikali na wadau wa mpira wa miguu walifanikisha hili haswa katika mchezo wa mwisho dhidi ya Uganda.

Msemaji wa TFF Clifford Ndimbo akiwa kwenye majukumu yake katika mchezo wa Tanzania dhidi ya Uganda

U-20 Kwenda Eritrea

TFF ilipokea mualiko wa mchezo wa kirafiki wa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kutoka kwa wenzao wa Eritrea. Na TFF haikusita kupeleka timu ya vijana chini ya mwalimu Juma Mgunda kutokana na mchezo huo kua ndani ya kalenda ya FIFA ya michezo ya Kimataifa.

Serengeti Boys kualikwa Rwanda

Katika kujiandaa na michuano ya Afcon ya vijana TFF ilipokea mualiko kutoka shirikisho la Rwanda kwenda kushiriki michuano maalum ya vijana chini ya miaka 17 yaliyoshirikisha nchi 3 tu yaani Rwanda Tanzania na Cameroon. Katika michuano hiyo Tanzania iliobuka kidedea baada ya kuifunga Cameroon mabao mawili kwa moja na kutoka sare na wenyeji Rwanda kwa mabao matatu kwa matatu.

Rais wa TFF Wallace Karia

U-18 Kupata Mualiko Misri

Timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 ilipata mualiko nchini Misri kwenda kushiriki michuano maalum ya timu nne, TFF haikusita kuipa maandalizi ya kambi timu hiyo na kuipeleka Misri kwenda kushiri michuano hiyo yenye timu kama Algeria, Morroco na wenyeji Misri. Mashindano yatafanyika jijini Alexandria-Misri.

Twiga Stars kufuzu michuano ya Olympic.

Twiga Stars inakabiliwa na mchezo dhidi ya Congo DRC ili kufuzu kwa michuano ya Olympic iatakayofanyika nchini Japan. Ambapo TFF ilihakikisha Twiga Stars wanapata kambi nzuri kulekea mchezo huo wakiwa chini ya mwalimu Bakari Shime. Twiga stars wamecheza mchezo wakwanza uwanja wa Taifa na kupata sare ya mabao 2 kwa 2 na sasa ipo Congo ili kucheza mchezo wa marudiano.

Makundi ya michuano ya AFCON-U17 itakayofanyika nchini Tanzania April 2019.

Serengeti Boys Kushiriki Afcon

Tanzania ndie mwenyeji wa michuano ya vijana ya chini ya umri wa miaka 17. Hapana shaka Serengeti Boys wakiwa timu mwenyeji wameandaliwa vizuri ili kuleta ushindani na kuweza kuwapa furaha Watanzania. TFF imekua ikiiandaa timu hii tangu mwaka jana huku ikifanikisha kambi ndani na nje ya nchi. TFF imefanikisha Serengeti boys kuweka kambi Arusha na Dar lakini pia kushiriki michuano nje ya nchi kama Rwanda na Uturuki.

Michuano ya AFCON  U-17  

Hakika kwa hili TFF wanastahili pongezi kwa kuweza kubeba uenyeji wa michuano hii mikubwa ya vijana kwa ngazi ya Taifa. Hakika maandalizi yapo sawa na kwa ushirikiano wa TFF na Seriakali mashindano yatakwenda vizuri.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.