Kombe la Dunia

Ujio wa Infantino waja na neema kwa mashabiki

Sambaza....

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA limeongeza tiketi kwa Tanzania kwaajili ya fainali za kombe la Dunia zitakazochezwa Russia mwaka huu, kwa mujibu wa taarifa kutoka shirikisho la soka Tanzania, TFF.

Kwa shabiki yeyote anayetaka kwenda kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia awasiliane na idara ya mashindano ya TFF kwa utaratibu wa namna ya kupata tiketi hizo.

My Requests EN

Ngwe hii ya pili ya tiketi za Kombe la Dunia imefunguliwa Februari 15, 2018 na itafungwa Machi 12, 2018.

Ikumbukwe awali FIFA walitoa tiketi 290 kwa Tanzania ili kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia kabla ya zoezi hilo kufungwa mwezi Januari na sasa imefunguliwa ngwe nyingine ya tiketi hizo.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x