Ngassa
Tetesi

Uncle Ngassa aipa mkono wa kwaheri Yanga!

Sambaza....

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa maarufu kama “Uncle” ameamua kuwaaga mashabiki na klabu yake ya Yanga kwa ujumla kutokana na kuandika maneno katika ukurasa wake wa Instagram unaoashiria msimu ujao hatokua tena mchezaji wa Yanga.

Ngassa ama “Enjoy soccer” inaonekana ni miongoni mwa wachezaji 13 ambao Yanga inatarajiwa kuachana nao katika kipindi hiki baada ya Ligi kumalizika.

Mrisho Ngassa au mzee wa “Enjoy Soccer”

“Kwanza nitoe shukrani zangu kwa wote tuliokuwa pamoja katika kipindi chote, Yanga viongozi wangu mashabiki na wachezaji wenzangu kwa kikao kilichofanywa leo sitakuwa katika kikosi cha Yanga niwatakie mafanikio yalio mema. Enjoy soccer.” Ameandika Uncle Ngassa katika ukurasa wake wa Instagram.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.