Shirikisho Afrika

Waziri: Afrika Kusini ni salama kwa Simba!

Sambaza....

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewatoa wasiwasi mashabiki wa soka wanaotaka kwenda nchini Afrika Kusini kuishangilia Simba katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates kuwa watakuwa salama.

Mchengerwa ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili 21, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Mohamed Mchengerwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

“Niseme tu kwamba sisi kama Serikali tunafuatilia kwa karibu usalama wa timu na hivi ninavyoongea nimemteua msaidizi wangu Mkurugenzi wa Michezo ili aweze kuniwakilisha kusimamia hili.” Mohamed Mchengerwa

Simba itakuwa na mchezo wa marudiano na Orlando Pirates nchini Afrika Kusini baada yakuibuka na ushindi  mwembamba wa bao moja bila kwa Mkapa. 

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao pekee walilolipata katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates

Waziri huyo ameyasema hayo baada ya mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba Barbara Gonzalez kuomba ulinzi kwa serikali ya Tanzania kufwatia kauli tata aliyotoa kocha wa Orlando Pirates Mandla Ncikazi baada ya mchezo wa awali kumalizika.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.