EPL

Yajue haya machache kabla ya urejeo wa EPL.

Sambaza....

Baada ya kutokuwepo kwa mpira siku 100 kwa sababu ya janga la coronavirus, Aston Villa na Sheffield United  watafungua ukurasa mpya wa urejeo wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

Michezo itachezwa bila ya mashabiki ili kuendelea kuchukua hatua za kuzuia kesi yoyote zaidi ya virusi vya corona.

Jezi maalumu ikiwa na alama ya ❤ ili kuwapa heshima wahudumu wa NHS

Ukimya wa dakika moja kukumbuka wale ambao wamekufa na ugonjwa wa virusi vya corona utafanyika kabla ya mechi za kwanza, wakati beji zenye alama ya moyo kama  shukrani ya wafanyikazi wa NHS pia zitavaliwa kwenye jezi.

Kwa mechi 12 za kwanza za michezo iliyoanza tena, majina yote ya wachezaji nyuma ya mashati yatabadilishwa na kusomeka “Black Lives Life”. Hii inafuatia kifo cha George Floyd huko Marekani, ambacho kimesababisha maandamano duniani kote.

Zaidi ya raundi nane za upimaji kwa mara mbili kwa wiki kwa wachezaji wa Ligi Kuu, kumekuwa na matokeo chanya kutoka kwa vipimo 8,687.

Michezo yote 92 iliyobaki itatangazwa moja kwa moja, na mechi nne kuonyeshwa na kituo cha BBC mara ya kwanza kufanywa kuwa bure kwanda hewani kwenye TV duniani tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu mnamo 1992.

Sadio Mane akipongezana na Mo Salah

Liverpool wapo kileleni kwa alama 25 zaidi ya anaeshika nafasi ya pili ambae ni Manchester City. Majogoo hao wa Liverpool, wanaelekea kulinyakua taji la EPL kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30.

Vilabu vya Bornamouth, Norwich na Aston Villa vipo katika hatihati ya kushuka daraja na kuelekea Championship kutokana na alama ndogo walizokua nazo na kuwafanya kuburuza mkia katika msimamo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.