Stephen Aziz Ki
Tetesi

Yanga yataja siku ya kumtambulisha Aziz Ki!

Sambaza....

Kaimu mtendaji mkuu wa Klabu ya Yanga Senzo Mazingisa amesema ni swala la muda tuu kwa wao kutambulisha sajili mpya za msimu ujao.

Akizungumza na kituo cha redio cha Efm Senzo amesema sio muda mrefu watamtambulisha nyota kutoka Burkina Faso Aziz Ki.

Kiungo mshambuliaji wa Asec Memosa Stephen Aziz Ki akimuacha mlinzi wa Simba Mohamed Hussein

“Tutamtambulisha (Aziz Ki) sio muda mrefu tulishamalizana nae muda mrefu sana subiri utaona.” Alisema

Senzo Mazingisa pia alikanusha uvumi wa Fiston Mayele kusajiliwa na Kaizer Chiefs na kusema kuna wanahabari wanataka kuwachanganya.

Fiston Kalala Mayele.

“Hizo taarifa sio zakweli Mayele haendi popote tutakua nae msimu ujao. Kuna wanahabari wawili kutoka Ghana wanataka kutuvuruga.” Senzo Mazingisa.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.