Kombe la Dunia

Shamte apewe muda, yule Msuva hatari! Unamuelewa Mao?

Sambaza....

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilianza kampeni yake ya kutafuta tiketi ya kwenda Kombe la Dunia dhidi ya Burundi. Michuano hii maarufu duniani itafanyika nchini Qartar mwaka 2022. Taifa stars ikiwa chini ya benchi linaloongozwa na ‘Deiwaka’, Kaimu kocha mkuu Ndayiragije Etienne walipata sare ugenini kwa Taifa stars lakini ni nyumbani kwa Ettiene. Hapa mpwa wangu nimekuletea zawadi hii kutoka Bujumbura kuhusu wachezaji walivyocheza, twende sasa..

1 Juma Kaseja

..alikuwa makini kwa asilimia kubwa Sana, aliokoa michomo mingi aliweza kupanga vizuri safu yake ya ulinzi (oral-defence) pia alijua kufanya delay (kupoteza) ya muda kwa mbinu na uzoefu wake hasa kipindi cha kwanza.

Alifungwa goli kutokana na kuchoka kisaikolojia, kuanzia tukio la mapema la ugomvi wa nje uliofanya wasiingie katika vyumba vya kuvalia na kuruhusu mashambulizi ya mara kwa mara.

2 Ramadhani Shamte (Haruna )

Yupo kwenye kiwango bora kiuchezaji kwa sasa. Ni moja ya wachezaji wazoefu wanaozaliwa upya. Kwenye jukumu lake la mwanzo la kukaba kama mlinzi kamilili alifanikiwa, ingawa dosari zake zilikuwa zinakuja anapopata nafasi kuja kama mshambuliaji mualikwa. Mipira yake (kumwaga maji) au pasi zake hazikuwa sahihi, japo kutokuwa na muunganiko mzuri wa career (Uzoefu) yake hapa ndio chanzo kikuu cha kukosa kujiamini. Lakini Akipata muda zaidi atakuwa bora sana, hasa kama tutafuzu hatua ya makundi ambapo huchezwa mechi sita.

3 Gadiel Michael

Gadiel bwana alikuwa yupo poa japo, makosa madogomadogo kwenye eneo la kupiga mipira. Alipokuwa anapanda mbele ilikuwa safi, ila Mara nyingi mipira yake ilikuwa haina macho.

Alizidiwa pia katika uwezo wa kuruka mipira ya vichwa (jumping force) hii kama ni mvivu kiasili na kisha unakutana wapinzani wenye maumbo ya urefu basi kwako huwa na shughuli pevu. Kiujumla aliisaidia Sana timu ukiachilia mbali dosari hizo ndogo.

Soma kuhusu udhaifu na umuhimu wa Gadiel hapa… Nani chaguo sahihi kiufundi: Tshabalala/Gadiel? Sehemu ya Pili

4 Kelvin Yondani

Kiranja, huyo mchezaji ni mzoefu na si mkongwe, hakika alikuwa na utamu wake kwa kuwa yeye ni pure center back (mlinzi wa nyuma). Aliruka na washambuliaji wa Burundi mwanzo hadi mwisho, alianzisha mashambulizi vyema japo tatizo lao la ujumla ni kupanda na timu kutoka chini.

Mara kadha walikuwa wakiwapasia viungo wao, wamemaliza kazi japo model football (Soka la kisasa) haishauri hiyo. Waliobahatika kuona mchezo huu watakubaliana nami hakuvuka mstari wa kati kwa angalau mara tano katika mechi nzima, pamoja na hayo kazi yake ilikuwa nzuri sana yenye kupendeza

5 Erasto Nyoni

Huwa najiuliza atachuja lini, lakini kila siku anazidi kuwa (mcharo) mpya na mtamu. Hawa walitengeneza pembe tatu ya uzoefu (triangle) na
kutumia uzoefu wao. Alitumia kimo chake vyema, kubattle na wachezaji warefu wa Burundi.

Alianzisha mipira kwa kuombea pembeni mara tu mpira unapokuwa kwa kipa , ana uhakika (kujiamini) sana na yupo makini sana anapokuwa mpira, Japo uvulana haujamtoka kwa kutaka kudhalilisha wapinzani kwa kuwapiga chenga za maudhi na kanzu au kuwafanyia vitu vya mpira bila kuhofia risk (madhara) na muda wa matukio haya, kiufupi kazi yake ipo vizuri.

6 Jonas Mkude

Moja ya kiungo bora Sana, kijana ambaye yupo katika kilele cha ubora wake. Yupo na uwezo mkubwa wa kuutawala mpira (ball control) pia anaweza kupoza timu kwa sababu yupo taratibu. Ila mkweli wa vitendo, anajua kupiga pasi za nje na ndani (instep na outstep) pasi ya ulalo na ya mbele (width na horrizontal).

Japo si mzuri wa ku-drive kwa maana ya kukokota mpira kwa umbali wa mita juu ya kumi na tano, hivyo anakuwa kama mtu mwenye eneo lake la kucheza (himaya) kwa kuwa partner (Mwenzake) wake hawapandi basi naye anajikuta yuko nyuma na timu na ankuwa na tabaka au gap kati ya mabeki na washambuliaji. Japo kumpora mpira ni shughuli na anajua kugombea mipira ya aina yote na jumping force yake ipo juu sana.

7 Himid Mao

Ukimuangalia kwa haraka ni vigumu kuuona mchango wake wa moja kwa moja kwa kuwa hajajaliwa mbwembwe. Hana kabisa urembo (art ya uchezaji), lakini kwa jicho la kifundi alikuwa na machango mkubwa Sana pale dimbani.

Kinafasi anapangwa kama kiungo wa pembeni (no 7), lakini kimajukumu ni mkabaji waeneo (zone) pale kati na kudeal na yeyote anayepita katika eneo hilo. Kwa mechi hii haikumpa option (nafasi) nzuri ya kushambulia au kupiga mipira kama jukumu la winga linavyotaka. Alitolewa kutokana na kuchoka katika kutimiza wajibu mkubwa wa majukumu aliyopangiwa. Binafsi huwa naielewa sana shughuli yake na walimu wanashauriwa kuwa na wachezaji wa aina zote uwanjani.

8 Salum Abubakar (Sure boy)

Yes hakufanikiwa eneo moja tu, na bahati mbaya alichelewa kugundua kwenye physical battle suala lilikuwa juu yake. Kimo kifupi ukifananisha na wapinzani na eneo analocheza kuwa na msongamano wa watu (numerical superior) miguu mirefu, height ni silaha kubwa ya maeneo haya. Kinyume chake uwe na maarifa makubwa na kucheza kwa woga touch moja moja tu, kupepesa macho kabla haujaufikia mpira (macho ya kinyonga). Kufanya maamuzi kabla ya first touch na mwisho nikuusoma mchezo kadri muda unavyoenda na mahitaji yake hasa kubadilika kwa mbinu za wapinzani.

Alitoa mchango kwa kadri alivyoweza japo kwa position yake majukumu makubwa ni kiji-involve kwenye transition ya mipira na kumalizia kwa pasi msaada (assist).

9 Mbwana Samatta

Wakati Rigobert Song anacheza katika kikosi cha Cameroon, walikuwa wanamuuliza wakati wa kuimba wimbo wa taifa “he who sing a song of hope”? Yaani ni Mwanaume gani anayetuimbishia wimbo wa matumaini? Huyu ni nahodha wetu, yeye ndio mleta matumaini ndani hatari kwa wapinzani kila muda, nguvu yake, kwa maana ni yakuvutia, footwork yake, one against one yake inashiba skills kifupi ni complete striker!

Aongeze usahihi matumizi ya mipira atakuwa zaidi ya Samatta huyu nakumbuka kuwahi kushangilia goli lake moja la dead ball pale Chamazi dhidi ya Lesotho japo simjumuishi katika wapigaji wazuri wa mipira iliyokufa.

10 Simon Msuva

Professionalism (Uweledi) inambeba sana, hali ya kujiamini ni kubwa kwa kuwa anafahamu. Kwa hili pia wapinzaji wanamuogopa kwakuwa ana hali ya kujiamini sana (confidence) na ana uwezo wa kufunga na kupoteza nafasi pia.

Kupoteza nafasi ni kitu ambacho cha kawaida kwa mchezaji kandanda , japo kama ukimchunguza Msuva wastani wake 3:1 kwamba ili akufunge ni lazima apoteze nafasi kisha ajisahihishe kwa kufunga. Pamoja na wastani huo weka mbali na watoto , ni miongoni mwa ma-silent killer, anakufunga bila kutarajia.

11 Dilunga

Kiungo wa pembeni kipepeo (fly) good pace na vikorombwezo kibao. Makosa yake makubwa siyo developer (Mtengenezaji) haachi mpira moja moja na kwa haraka, ana kaa na mpira hata kwenye maeneo ambayo hapaswi kukaa. Ingawa ni nimzoefu lakini ana makosa ya wachezaji ya njuka wa form one katika careers.


12,13 ,14 Idd Nado, Domayo, Farid Musa walifanya vyema kwa kuwa walikuja kutokea nje ambako wameshatoa (Tension) timu inaturn katika ulinzi wa eneo na kwenda katika kujihami kwa kushambulia ambako ni rahisi sana kusema wamecheza vizuri.

Ukimwacha Nado ambaye ndio anakaribia climax (Kiwango chake cha juu) yake, Farid yupo kwenye climax yake anapaswa kupewa muda zaidi angalau dakika sitini 60 hivi anaweza kutoa mchango zaidi ya ule.

Benchi la Ufundi lote chini ya Ndayiragije kwangu ndio bora ki-mbinu na game approaching kiujumla yes walifanya kazi kubwa sana technical substitute nk. Kubadilika kwa mbinu mara kwa mara kadri ya mahitaji nk, nakadhalika. Ombi langu kwao ni kuijenga timu vizuri ikacheza mechi hizi za mtoano kwa nguvu na maarifa mengi kisha tukafuzu makundi ambako pressure yake si kubwa ukifananisha na mtoano.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x