Ahmad Ahmad (Kulia) wakifuatilia mechi ya AFCON U17 viwanja vya Chamazi, Dar es Salaam.
Stori

Apewe Maua Yake Sio Mpaka Aondoke!

Sambaza....

Sipo hapa kupiga kampeni kuhusu uchaguzi mkuu wa TFF, wala sipo hapa kuzungumza kuhusu mapungufu ya uongozi wa sasa wa TFF sababu sio lengo langu kwa leo, mimi nipo hapa kupongeza uongozi wa TFF chini ya Wallace Karia.

Vizuri! Mapungufu hayawezi kukosekana sababu tupo kwenye Dunia ambayo inahitaji tujifunze vitu vipya kila siku hivyo ni ngumu kuepuka makosa pale unapojifunza ndio Ulimwengu ulivyo.
1
Tafadhali acha mrejesho hapax

Walace Karia namuona kama mshindi kwenye mpira wetu, kuna njia ya thamani sana anaitengeneza ili tupite na kufika tunapotaka kwa haraka zaidi! Inapendeza sana kwa Utawala wake huu kuona mpira wa miguu Tanzania unapiga hatua kubwa sana.

Kuanzia kwenye Kandanda la Wanawake ameweka nguvu kubwa sana iliyofanya walau kupata muundo mzuri wa Ligi Kuu ya Wanawake inazidi kupiga hatua kila siku, hii imefanya Klabu kama Simba Queens kucheza Klabu Bingwa ya Wanawake huku JKT Queens wao ni msimu  huu.

Simba Queens Mabingwa wa kombe la Cecafa msimu 2022-2023.

Timu za Taifa za Wanawake zinafanya vizuri sana kwenye mashindano ya Afrika, muundo mzuri wa Ligi yetu ya Wanawake umeanza kulipa sana ndio maana Klabu zimeanza kufanya usajili was wachezaji wakigeni kwenye Ligi Kuu ya Wanawake.

Taifa imeenda Afcon mara ya pili kwenye utawala wake achilia mbali ushiriki mzuri wa Klabu zetu kwenye michuano ya CAF! Hapo sijazungumza kuhusu vituo vya kandanda vinavyojengwa mikoa tofauti tofauti kwaajili ya kuendeleza kandanda letu.

Tumeomba kuandaa Afcon 2017, mikutano mikubwa ya kandanda pia imefanyika Tanzania yenye faida kubwa kwa mpira wetu! Vipi kuhusu fainali za ASFC ambazo zinachezwa mikoani lengo lake ikiwa ni kuusambaza mpira wa miguu mpaka kule ambapo watu waliusahau mchezo huu pendwa.

Rais wa TFF Wallace Karia.

Udhamini wa Ligi Kuu, hapa thamani inazidi kuongezeka makampuni yamekuja kuweka pesa kwa sasa Ligi yetu inatangazwa redioni na kuonekana kwenye luninga vizuri sana, mikoani mechi zinachezwa usiku, Championship nayo njia zinafunguka mechi kadhaa msimu uliopita zimeoneshwa kwenye luninga.

Bora utoe pongezi pale mtu anapofanya vizuri na usisubiri mpaka aondoke ijapo mapungufu yapo pia. Lakini hapa kila mtu anaona kazi ni kubwa sana inafanywa na inaonekana

Endelea kufanya Rais Wallace Karia.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

1 Gumzo
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
Acha ujumbe hapa Vizuri! Mapungufu hayawezi kukosekana sababu tupo kwenye Dunia ambayo inahitaji tujifunze vitu vipya kila siku hivyo ni ngumu kuepuka makosa…" Read more »

Hakika ameitendea haki soka la Tanzania

1
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x