Sambaza....

Yanga SC, ipo katika harakati za kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi Mwenyekiti wa klabu hiyo, kuelekea huko tayari Katibu wa baraza la Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali, ameonesha nia ya kuitaka nafasi hiyo

Akilimali ameonesha nia ya kuwania nafasi hiyo, iliyokosa mtu kwa muda mrefu tangu kujiuzuru kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Mahboob Manji

Katibu huyo amefafanua kuwa, klabu hiyo inapitia kipindi kigumu kwa sasa hivyo ameonelea ni vema akagombea nafasi akieleza anaweza kuinasua katika matatizo iliyonayo kwa sasa

Kutokana na hali hiyo Akilimali “Abramovich” amesema ni muda sahihi sasa kwa klabu hiyo kutoka katika hali waliyonayo ya kukosa pesa na kurejea kama zamani walipokuwa vizuri kifedha

Sambaza....