Sambaza....

Yanga na Azam FC zinatenganishwa na bao moja na ushindi mmoja pekee katika rekodi zao za muda wote katika mashindano yote. Bao linalowatenganisha lilifungwa dakika ya 70 ya mchezo wao wa Aprili Mosi, 2017 na Obrey Chirwa.

Rekodi ya Yanga dhidi ya Azam FC

Kwa hiyo mchezo huu utakuwa VITA ya kulinda bao kwa Yanga au kusawazisha kwa Azam FC.

LIGI KUU

Timu hizi zimekutana mara 18 kwenye Ligi Kuu tangu zilipokutana kwa mara ya kwanza, Oktoba 15, 2008. Yanga imeshinda mara 6, Azam FC imeshinda mara 5 na zimetoka sare mara 7. Yanga imefunga mabao 26 na Azam FC imefunga maba 25.

Endapo Azam FC itashinda 1-0, timu hizi zitalingana kila kitu kwenye ligi kuu.

MASHINDANO YOTE

Timu hizi zimekutana mara 31 kwenye mashindano yote. Yanga imeshinda mara 12, Azam FC imeshinda mara 11 na zimetoka sare mara 8. Yanga imefunga mabao 41 na Azam FC imefunga mabao 40..

Endapo Azam FC itashinda 1-0, timu hizi zitalingana kila kitu kwenye mashindano yote

Sambaza....