Ligi

Habari za Ligi Kuu maarufu Duniani Ligi Kuu (Premier League) hivyo hapa tunakuletea mkusanyiko wa uchambuzi na matukio yanayohusu Ligi Kuu pekee pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara (Ligi Kuu)

Ligi Kuu

Tathimini ya mchezo Simba vs Singida United

Kwa hakika ulikuwa mchezo mzuri na wenye ushindani wa kiufundi kwa timu zote mbili. Simba wakitumia tactical deployment 3-5-2 walionekana kumiliki mpira kwa kiasi fulani kuanzia kwenye eneo lake la kiungo, tofauti na michezo iliyopita kwenye mchezo wa leo simba walionekana kuimalika vema kwenye mfumo na aina yao ya uchezaji....
Ligi Kuu

Kocha wa Simba SC huyu hapa!

Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya,Mfaransa Pierre Lechantre, kwa mujibu wa taarifa kutoka msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara. Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu...
La Liga

Kwaheri fundi Ronaldinho Gaucho

Tarehe 21, Machi 1980 kunako mji wa Port Alegre nchini Brazil mtoto Ronaldo de Assis Moreirra alizaliwa, mzee Joao Moreirra na mkewe Bi Miguerina De Assis walifanikiwa kumzaa mtoto ambaye baada ya miaka kadhaa kupita alifanikiwa kuwa mwandinga maarufu Jina lake halisi anaitwa Ronaldo lakini wabrazil ili kumtofautisha na Ronaldo...
Ligi Kuu

Licha ya sare, Lwandamina alikuwa jukwaani tu

Kocha mkuu mabingwa watetezi wa ligi ya soka Tanzania bara Yanga sc, George Lwandamina, leo hii ameshuhudia kikosi chake kikigawana alama na Mwadui Fc akiwa jukwaani Lwandamina alikuwa jukwaani na baadhi ya viongozi wa Yanga katika kile kilichoelezwa kuwa kibali chake cha kufanyia kazi nchini kimekwisha muda wake "Bado tunaendelea...
Ligi Kuu

Bernabeu Ilisimama, Leo Dunia imesimamishwa kichwa

Hakuna kitu kigumu kama kucheza katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Uwanja ambao wachezaji nguli washapita pale na kuweka rekodi nyingi za soka duniani. Uwanja ambao una mataji mengi ya kombe la klabu bingwa barani ulaya. Kombe ambalo lina ushindani mkubwa lakini wao ndiyo Wafalme kwa kulichukua. Wao ndiyo waliochukua mara...
Ligi Kuu

Kisiga anaishi kijamaa katika dunia ya kibepari

Shaban Kisiga Malone. Mchezaji mmoja na nusu. Dead ball specialist. King of assist. Ball player. Ally Kamwe aliwahi kuniambia anachoweza kukifanya Said Juma Makapu kwa dakika moja, Kisiga anakifanya kwa sekunde mbili. Huyu ndiyo Kisiga aliyeamua kuukacha mpira na kukaa zake Vingunguti. Jumamosi asubuhi nilikuwa nikifuatilia mahojiane yake na kaka...
LigiLigi Kuu

Yanga yasaini mkataba na Macron

Klabu ya soka ya Yanga leo hii imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya Macron wenye thamani ya shilingi za kitanzania bilioni 2, kwa ajili ya utengenezaji na uuzaji wa jezi za klabu hiyo Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo leo makao makuu ya klabu hiyo, yaliyopo...
Ligi Kuu

Kiyombo geuka nyuma umwangalie Bahanuzi

Hapana shaka umepata sifa nyingi, kila mtu anafurahia kutaja uwezo wako mahiri. Mwingine atasema unajua kutumia miguu yote miwili. Huyu akaja na jambo lake la wewe kuwa na uwezo mkubwa wa kufunga magoli ya mbali kwa mashuti makali. Tena huyu atamalizia kwa kusema anafunga magoli ya kiume. Ili mradi tu...
Ligi Kuu

Viongozi wa Simba, Ndanda fc wapelekwa kamati ya maadili

Sekretarieti ya shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya maadili viongozi wanne kwa kughuhushi na udanganyifu Viongozi walioshtakiwa kwenye ya Kamati ya maadili ni msimamizi wa kituo cha Mtwara Dunstan Mkundi, Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Mtwara Kizito Mbano, muhasibu msaidizi wa klabu ya...
Ligi Kuu

Chirwa anahitaji Msaada

Sina tatizo na Tff wala kamati zake na hata muda uliotumika kupitia vielelezo pia naona ulikuwa sahihi kabisa kutokana na uhalisia wa jambo lenyewe Ndio ilikuwa sahihi kwa maana Obrey Chirwa aliitwa na Tff, lakini alikuwa kwao Zambia akifanya shughuri zake za kilimo na hata aliporudi nchini aliunganisha Zanzibar kwenye...
1 112 113 114 115 116 118
Page 114 of 118