LigiLigi Kuu

Yanga yasaini mkataba na Macron

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga leo hii imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya Macron wenye thamani ya shilingi za kitanzania bilioni 2, kwa ajili ya utengenezaji na uuzaji wa jezi za klabu hiyo

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo leo makao makuu ya klabu hiyo, yaliyopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa “master” amesema kuwa mkataba huo utakuwa na ongezeko kutokana na makubaliano waliyofikia

“Dau litakuwa likiongezeka kulingana na mauzo ya jezi za mashabiki” alifafanua Katibu huyo

Hiyo sio mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kuwekeza katika soka la Tanzania, itakumbukwa kuwa mwishoni mwa mwaka jana walisaini mkataba na shirikisho la mpira Tanzania TFF kwa udhamini wa jezi za timu za taifa wenye thamani ya shilingi milioni 800.

Kwa udhamini klabu ya Yanga sasa itakuwa imejiongezea wadhamini baada ya wale wa awali kampuni ya michezo ya ubashiri ya SportPesa.

Katika hatua nyingine hafsa habari wa klabu hiyo Dismas Ten, alizungumzia maandalizi yao kuelekea katika mchezo wa kesho wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, dhidi ya Mwadui FC utakafanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam

Dismas Ten alisema kuwa katika mchezo huo watawakosa wachezaji wao watatu walio majeruhi

“Tunawachezaji wetu ambao bado ni wagonjwa, Geoffrey Mwashiuya, Thaban Kamusoko na Donald Ngoma hao wataukosa mchezo huo pamoja na Obrey Chirwa anayetumikia adhabu iliyotolewa na kamati ya nidhamu” alisema Ten

Aidha Dismas Ten amewataka wapenzi na mashabiki wa klabu kujitokeza kwa wingi kuisapoti klabu yao.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x