Sambaza....

Liverpool imetinga fainali Ligi ya mabingwa wa Ulay licha ya kichapo cha mabao 4-2 walichokipata kutoka kwa AS Roma, Majogoo hao wamefudhu kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-7 ikiwa ni fainali yao ya 8

Mabao ya Liverpool, yalifungwa na Sadio Mane na Giorgio Wijnaldum, hivyo itakutana na Real Madrid katika mchezo wa fainali mjini Kiev

Real Madrid ndio ilikuwa ya kwanza kufudhu hatua ya fainali, baada ya kuwaondosha Bayern Munich kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3

Dejan Lovren of Liverpool lifts a red scarf over his head as he celebrates in front of the Liverpool fans at the Stadio Olimpico

Bao alilofunga Sadio Mane linaifanya safu ya ushambuliaji ya Liverpool kufikisha mabao 29, katika UCL, bao moja zaidi waliyofunga Karim Benzema, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo msimu wa mwaka 2013/14 wakifunga mabao 28

Bao la kujifunga la James Milner, linakuwa bao la kwanza kwa Liverpool kujifunga tangu beki John Arne Riise afanye hivyo katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Chelsea msimu wa mwaka 2007/8

Bao la Edin Dzeko linakuwa bao la tano kufunga mfululizo katika mechi 5 za msimu huu wa UCL, na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa AS Roma kufunga mabao 5 katika mechi 5 mfululizo ya UCL

Sambaza....