Blog

George Weah acheza dakika 79, mechi ya kirafiki dhidi ya Nigeria

Sambaza....

Rais wa Liberia George Weah mwenye umri wa miaka 51 jana Jumanne amecheza dakika 79 katika mchezo wa kirafiki kati ya Taifa lake na timu ya Taifa ya Nigeria mjini Monrovia.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya kuistaafisha jezi namba 14 ambayo ilikuwa ikivaliwa na George Weah katika kipindi ambacho alikuwa akiitumikia timu yake ya Taifa, ilishuhudia Liberia wakifungwa mabao 2-1.

Mchezaji huo wa zamani wa AC Milan aliapishwa kuwa Rais wa 25 wa Liberia mwezi Januari mwaka huu.

Katika mchezo huo Nigeria waliwaanzisha wachezaji wote muhimu kama mshambuliaji wa Leicester City Wilfred Ndidi na Peter Etebo wa Stoke City, huku Kelechi Iheanacho akiingia kipindi cha pili.

Mabao wa Nigeria yalifungwa na Simeon Nwankwo ambaye alionganisha mpira wa kona wa Peter Etobo baada ya mchezaji wa Galatasaray Henry Onyekuru kufunga bao la kuongoza.

Liberia walipata bao lao katika dakika za mwisho baada ya Rais George Weah kutoka, kwa njia ya Penati iliyofungwa na mchezaji wa zamani wa Yanga Kpah Sherman.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x