Ligi Kuu

Jembe Ulaya alia na Kessy

Sambaza....

Beki wa zamani wa Yanga sc, na timu ya taifa ya Tanzania Bakari Malima “Jembe Ulaya” amemtolea lawama mlinzi Hassan Ramadhan Kessy kufuatia kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya mahasimu wao Simba

Jembe Ulaya

Kessy, alitolewa nje kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano na mwamuzi baada ya kumchezea rafu mlinzi wa Simba, Asante Kwassi ikiwa ni mapema kabisa kipindi cha pili cha mchezo huo

Akizungumzia tukio hilo, Malima amesema kuwa Kessy bado ana utoto mwingi hali inayoweza kuighalimu timu katika michezo yake

Faulo iliyopelekea Kessy apate kadi

Alikielezea kitendo alichofanya Kessy, kuwa sio cha kiungwana na alipaswa kuwa mtulivu uwanjani sio kuonesha mpira wa ajabu uliopelekea atolewe mchezoni na mwamuzi

Pia Malima, aliielezea timu yake hiyo ya zamani kuwa ilicheza vibaya na Simba walistahili ushindi huo kutokana na mchezo waliocheza

Malima, enzi zake alisifika kwa kucheza soka la kasi, nguvu na maarifa hali iliyopelekea kuchukuliwa na klabu ya Vaal professional ya Afrika kusini

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x