BlogMabingwa Ulaya

Kane: Sihitaji mapumziko, mbona nipo Fit!

Sambaza....

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tottenham Hotspurs,  Harry Kane amesema anajisikia yupo fit pengine kuliko wakati wowote licha ya kuanza taratibu kwenye ligi kuu soka England .

Kane ambaye msimu uliopita alifunga mabao 41, yakiwemo 30 ya kwenye ligi ya England, amefunga mabao mawili tu katika mechi tano ambazo amecheza mpaka sasa, jambo ambalo wachambuzi wengi wa soka walishauri mshambuliaji huyo apewe muda wa kupumzika.

Baada ya mchezo dhidi ya Liverpool ambao ulishuhudia Tottenham wakipoteza kwa mabao 2-1, Kane alilizungumzia hilo na kusema kuwa japokuwa ni kweli amecheza mechi ikiwemo kuisaidia England kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia lakini hajisikii kuchoka na wala haitaji kupumzika ili aweze kuwa fit tena.

“Watu mara nyingi wanatafuta sababu hasa pale unapokuwa mtu muhimu kwenye timu na mtu ambaye unatakiwa kufunga mabao, kama timu tunacheza pamoja lakini ukiwa mshambuliaji unazungumziwa sana, lakini najisikia imara zaidi, kama nisingekuwa kocha nisingejichagua kucheza, ananiamini, najiamini na pengine naweza kufunga mabao kwenye mechi ya Jumanne,” Kane amesema.

Kane mwenye umri wa miaka 25 amesema atawajibu wachambuzi wanaoshauri kupumzika katika mchezo wa kundi B wa Ligi ya Mabingwa ulaya dhidi ya Inter Milan siku ya Jumanne.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x