Sambaza....

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania “Taifa stars “, Mzanzibar Hemed Suleiman “Morocco”, amesema kuwa maandalizi yao ya mchezo wa kesho dhidi ya Congo yamekamilika yameenda vizuri lakini akaweka wazi kuwa mchezo hautakuwa mwepesi.

Kocha huyo, ameyasema hayo ikiwa imesalia siku moja kabla ya mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki wa kalenda ya FIFA, unaotaraji kupigwa kunako uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam.

Morocco ametanabaisha kwamba Stars itawakosa wachezaji wake wawili Abdulaziz Makame na golikipa Aishi Manula.

 

“Tutawakosa wachezaji wetu Aishi Manura ambaye bado hajapona majeraha yake, hivyo golikipa aliyedaka dhidi ya Algeria ataendelea kuwa golini kesho, pia Makame hatoweza kucheza baada ya kuumia mazoezini”

Itakumbukwa kuwa Mohammed Abdulrahman ndiye aliyedaka katika mchezo dhidi ya Algeria, ambapo aliruhusu mara nne mipira kutinga kunako nyavu zake.

Aidha Morocco, amesema kuwa lengo lao ni kushinda katika mchezo huo ili kujiweka pazuri kunako viwango vya ubora vya FIFA.

Sambaza....