Sambaza....

Uongozi wa klabu ya Singida United, umeamua kuwapa zawadi mashabiki wake kwa kuwapa fursa ya kuingia bure katika mchezo wao wa kesho wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam sports Federation Cup (ASFC)

Singida United, inataraji kushuka kunako uwanja wake wa nyumbani wa Namfua Stadium kuwakaribisha maafande wa JKT Tanzania

Akizungumzia mchezo huo mtendaji wa Singida United, Festo Sanga, wameamua kulipia mchezo huo ili mashabiki wao wengi waingie uwanjani kuishangilia timu hiyo

“Ni kweli kesho Singida United tuna mchezo mkubwa dhidi ya JKT Tanzania, na tutaingia katika mchezo huo kwa tahadhri kubwa kutokana na matokeo waliyopata JKT”

“Tupo tayari kwa mpambano dhidi JKT, niwaambie mashabiki kuwa kikosi kipo kamili huku tukiwakosa wachezaji wawili ambao wanatumikia adhabu”

Pia mtendaji huyo, alifafanua zaidi kwa kusema kuwa uongozi wa Singida United umeamua kulipia mchezo huo ili kutoa zawadi kwa mashabiki wake waingie bure

“Kikubwa zaidi sisi uongozi wa Singida United, tumeamua kuwapa zawadi mashabiki waingie bure, tumelipia na tumefata taratibu zote za TFF”

Timu ya Singida United, imenuna mchezo kwa maana mashabiki wataingia bure, hivyo tunawaomba mashabiki waje kwa wingi ili kuisapoti timu yao” aliongeza Mtendaji huyo

Mshindi katika mchezo huo, atakutana na Mtibwa sugar katika mchezo wa fainali ikitaraji kupigwa Juni 2, 2018 kunako uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha

Sambaza....