Khalid Aucho katikati ya wachezaji wa Azam Fc
ASFC

Ni Vita Nyingine ya Rekodi Leo.

Sambaza....

Tarehe 12 mwezi huu katika dimba la CCM Mkwakwani mkoani Tanga unachezwa mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho la Azam (Azam confederation cup), mchezo huo utawakutanisha Yanga Sc na Azam Fc.

Azam walifanikiwa kutinga fainali baada ya kuwatoa Simba sc katika mchezo wa nusu fainali kwa jumla ya mabao 2-1 katika dimba la Nang’wanda Sijaona mkoani Mtwara huku Yanga wakicheza na Singida Big Stars katika uwanja wa Liti mkoani Singida na kuibuka washindi katika mchezo huo wa nusu fainali na kutinga fainali.

Azam na Yanga wanapokutana mchezo unakuaga mgumu sana na katika michezo yao mitano ya hivi karibuni iliyowakutanisha wababe hao Yanga kushinda 3, sare 1 huku Azam akishinda mara 1 pekee.

Abdul Sopu akimuacha Salum Aboubacar “Sure Boy”.

Katika msimu huu wa ligi ya NBC uliotamatika Yanga amemaliza nafasi ya kwanza huku akiwa kinara na kufanikiwa kuwa bingwa wa ligi hiyo huku Azam akifanikiwa kumaliza ligi katika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Simba.

Mechi hiyo ya fainali inatarajiwa kuwa kali na yakibabe sana kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote mbili, Azam wanajinasibu kupambana kufuta uteja mbele ya Yanga na kuweka rekodi mpya huku Yanga wakijinasibu kuendeleza ubabe wake mbele ya Azam.

Mchezo unatazamiwa kuwa  mgumu kiasi kwamba joto la mchezo huo miongoni mwa mashabiki liko juu na timu zote zikiwa tayari kwa mchezo. Azam anautaka ubingwa kwani mara ya mwisho aliuchukua mbele ya Lipuli  katika mchezo wa fainali na ilikua mwaka 2019.

Kombe la FA.

Ni miaka minne imepita sasa Azam Fc wamefanikiwa tena kutinga fainali akionekana mwenye uchu na njaa ya kombe hilo lakini sio rahisi kwani Yanga wanataka kumaliza msimu huu wa mashindano katika ubora mkubwa baada ya kufanikiwa kuchukua ligi.

Mkwakwani iko tayari, Wanatanga wako tayari, Dunia na wapenzi wote wa soka wako tayari kushuhudia fainali hii ya kibabe ya kuendelea kuweka na kuzivunja rekodi.

NB:Ng’ombe kakosa ndevu ila mbuzi kapewa.


Sambaza....