ASFC

Kuondolewa kwa timu kubwa kwenye kombe la FA hakuhusiani na kushuka kwa viwango

Sambaza....

Binafsi naomba kwanza nizipongeze timu zote zilizofanikiwa kuingia hatua hii ya nusu fainali ya michuano ya kombe la FA, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC)

Tukirudi nyuma kidogo ebu tujiulize hivi kwa nini mashindano haya yalianzishwa katika ulimwengu wa Soka ?

Nchini Uingereza kombe la shirikisho au FA cup ni moja ya mashindano kongwe nchini humo mashindano haya yalianzishwa mnamo mwaka 1871 na hadi kufikia mwaka 2011-2012 zilishindanishwa zaidi ya timu 763, na hufanyika droo 12, hadi kufikia nusu fainali

Timu za madaraja ya chini hushindana kwa mtoano hadi kufikia idadi ya timu 32, zinazojiunga na timu 48, za daraja la kwanza na la pili na katika droo ya mwisho ndio zinaingia timu za ligi kuu

Hapa lengo nini kuhamasisha timu ndogo nazo zitumie fursa hiyo ya kombe la shirikisho kujitangaza kwani wakijipanga vema wanaweza kupata ushindi wa MAAUAJI MAKUBWA basi hii inakuwa njia rahisi kwao kujitangaza

Na ili kuhamasisha zaidi ukifanikiwa kuchukua kombe basi ujue wewe si timu ndogo tena una uwezo kuwakilisha nchi

Ukiangalia mtililiko wote na umefanikiwa kuchukua kombe basi utakua una timu nzuri na una haki ya kuwakilisha nchi kunako michuano ya kimataifa

Japo tathimini iliyofanyika nchini Uingereza kunako michuano ya FA, kombe hili ni asilimia chache sana timu za madaraja ya chini kufika fainali japo asilimia 99.85 inaonyesha timu moja ndogo yenye bahati na kuongeza jitihada inaweza kuifunga moja ya timu 6 bora kwenye msimamo wa ligi kuu katika msimu huo

Hapa sio ajabu au sio kushuka viwango vya timu kubwa, ama timu ndogo kuwa na misuli ya kiuchumi hapana hali hii hutokea sehemu yoyote yanapofanyika mashindano kama haya kwa faida ile ile ya mtoano wakiwa na bahati yao basi wanaweza kupata ushindi unaoitwa GIANT KILLING VICTORY

Na zipo timu zenye uwezo mdogo kifedha zinaweza kuchukua kombe kutokana jitihada zao ikichagizwa na bahati pia, ila ikifikia suala la kuwakilisha nchi hushindwa kufanya hivo nafasi yake huchukuliwa na timu yenye uwezo mzuri kiuchumi

Mfano nchini Angola msimu wa mwaka 2015 timu ya Onze Bravos, ilifanikiwa kuchukua kombe la FA la nchi hiyo ila walishindwa kuwakilisha nchi kunako mashindano ya kimataifa kutokana na kutokuwa vizuri kiuchumi, na nafasi hiyo ikapewa timu ya Sagrada Esperança iliyoondolewa na Yanga sc kunako michuano ya kombe la shirikisho Afrika

Kwa kuhitimisha hili, mashindano haya huwa hayahusiani na kushuka kwa viwango kwa timu vigogo ama timu ndogo kuwa na uwezo kiuchumi

Kuna wakati bahati inaweza kuchukua nafasi yake kunako michuano hii, na kuleta matokeo ya kushitua wengi kwa kuondoa timu kubwa ambayo ipo katika kiwango kikubwa bora

Mfano simba walivyotolewa na timu ya Green Warriors sio kwamba Simba walikuwa kwenye kiwango kibovu

Manchester city ya nchini Uingereza, pia yaliwakuta kama yaliyowakuta Simba na Yanga hivi ndivyo yalivyo mashindano haya

Lakini pia bila kusahau mchezo soka una tabia zake, na moja kati tabia hizo ni kutoa matokeo ya kustaajabisha ambayo hayakutarajiwa na wengi, hii ni tabia ambayo hufanya mchezo huu uwe wa kuvutia na unaopendwa na wengi.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x