Sambaza....

Kuelekea mchezo wa kombe la shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Yanga sc hapo kesho, klabu ya Majimaji FC itawakosa nyota wake watano

Hafsa habari wa klabu hiyo, Onesmo Ndunguru, amesema kuwa kikosi chao kitawakosa jumla ya wachezaji watano wenye matatizo mbalimbali, hivyo benchi la ufundi la timu hiyo kutumia wachezaji wa kikosi cha pili kwenye mchezo huo

Akiongea na mwandishi wa Website ya Kandanda, Hafsa habari huyo aliwata wachezaji watakaokosekana kwenye mchezo huo kuwa ni Kennedy Kipepe, Paul Maona, Andrew Ntala, Sixmund Mwasekaga na Sadiq Giawaza

“Kocha amepanga kuongeza wachezaji wa kikosi cha pili, kwa sababu atawakosa wachezaji watano wa kikosi cha kwanza” alisema Hafsa habari huyo

Pia Hafsa habari huyo amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuishangilia timu yao itakapokuwa inaisambaratisha Yanga

“Tumepanga kulipa kisasi cha kufungwa mabao 4-0 kwenye mchezo ligi kule Dar es salaam, hivyo lengo letu ni kuiondoa Yanga kwenye michuano hii” alisema Onesmo

Itakumbukwa kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu kunako uwanja wa taiga jijini Dar es salaam Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0

Sambaza....