Ligi Kuu

Masoud Djouma amkaribisha Okwi

Sambaza....

Kocha wa Simba sc Masoud Djouma, amezungumza na mchezaji wake Emmanuel Arnold Okwi na huenda leo asubuhi akaanza mazoezi na wenzake

Kiungo mshambuliaji huyo ameungana na kambi ya Simba iliyopo Morogoro, wakijiandaa na mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Singida United

Okwi aliyewasili nchini leo akitokea kwao Uganda na kujiunga na wachezaji wenzake huko Morogoro maarufu kama mji kasoro bahari

Mapema wiki kadhaa zilizopita kocha huyo alikaliliwa kutofurahishwa na uchelewaji wa mchezaji huyo, lakini leo wamezunguza vizuri na kesho huenda mchezaji huyo akaanza mazoezi na wenzake huko Morogoro


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.