Sambaza....

Michezo ya nusu fainali ya Azamsports FederationCup tayari imepangiwa tarehe. Michezo hiyo itapigwa April mwaka huu,  zikizihusisha timu nne zilizifuzu hatua hiyo ambazo ni Singida utd, Mtibwa Sugar, Stand UTD na JKT Tanzânia.

Mchezo wa kwanza wa nusu fainali utapigwa tarehe 20 April mwaka huu katika dimba la Kambarage Shinyanga ambapo Stand UTD itaikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Mchezo wa pili wa nusu fainali utapigwa tarehe 21 April mwaka huu katika dimba la Namfua ambapo Singida utd itaikaribisha JKT Tanzânia.

Fainali ya Azamsports FederationCup itapigwa May 31 katika uwanja utakaotajwa hapo baadae.

Sambaza....