Sambaza....

SOKA ni mchezo unaoongozwa na historia huwezi kuiona thamani ya mchezo huu usiporudi katika historia, wengi wetu tumekuwa ni watu wakutoamini historia katika soka tukidhani kwamba ni kupoteza muda lakini si hivyo na tunavyo amini, maana mengi yanayofanywa sasa yanatoka katika historia za nyuma

Tumeona wanasoka wengi ambao wanahitaji kuwa bora au tayari wamekuwa bora, kitu pekee ambacho huwa kina wabeba ni kufuta zile rekodi za wanasoka wa zamani na kuandikab zao, ni iko hivyo maana ukihitaji kuwa bora tafuta zile ambazo zilikuwa katika historia,vunja zile alafu tengeneza yako lazima utakuwa bora zaidi

Unaikumbuka miguu ya Mholanzi mmoja aliyetokea PSV na kujiunga na Manchester United miaka ya 2001, medani ya soka ilimtambua kwa jina la Ruud Van Nistelrooy, uhodari wa miguu yake katika ufungaji iliweza kuwashtua akina Alan Shearer na Thiery Henry ambao wao nao walikuwa hawa tofautiana sana aina ya uchezaji wao.

Van Nistelrooy alikuwa ni mfungaji, maana alilitambua vyema goli zaidi ya golikipa, alikuwa na wastani mzuri wa kufunga kulingana na mechi ambazo atakuwepo uwanjani, wakati anajiunga na United katika msimu wake wa kwanza aliweza kufunga idadi ya mabao 23 katika michezo 32 ya ligi kuu na ndipo akaleta tafrani kwa watu kama Henry na Shearer.

Kumbuka huo ulikuwa msimu wake wa kwanza, msimu wa pili ukaonekana ni rahisi sana kwake maana tayari alishaweza kuwa juu ya ligi, aliweza kushinda kiatu cha mfungaji bora pamoja na mchezaji bora wa msimu akiwa na United, lakini aliweza kushinda tena tuzo za mchezaji bora wa mwezi mara tatu ndani ya msimu, hiyo ndio miguu ya Kiholanzi

Katika dhama hizi tumepata mtu wa aina ile ya Van Nistelrooy, mtu mwenye miguu ya Kiholanzi lakini sura ya Kiarabu ya kutoka kule nchini Misri huyu ni Mohammed Salah, nadhani hapa historia inaweza kutengenezwa na kuisahau ile ya Van Nistelrooy na ndio maana awali nilieleza kwamba soka ni mchezo unaongozwa na historia.

Salah ni aina ya mfungaji ambaye anaufanya mchezo wa mpira wa miguu uonekane mwepesi hasa katika nafasi yake ambayo anacheza, amekuwa na wastani bora sana wa kufunga, na hii leo ni rahisi kuuliza Salah amefunga magoli mangapi kuliko kusema Liverpool imepata ushindi wa aina gani

Huu ni msimu wa kwanza kwake katika klabu ya Liverpool tangu alipojiunga akitokea AS Roma ya kule Italia mpaka sasa amecheza michezo 30, katika Premier League na katika michezo hiyo tayari amefunga mabao 24, hapo hapo  tayari Salah ameshinda tuzo tofauti tofauti katika msimu huu bila kuisahau ile aliyoshinda mwezi Novemba ya mchezaji bora wa mwezi

Sura hii ya kiarabu naweza nikasema kwamba bado miguu yake itaendelea kutuonyesha ubora ule ambao Van aliweza kuufanya ndani ya Premier League katika misimu 6 ambayo alikaa na United, pia nadiriki kusema kwamba ni rahisi sana tena kuiona tuzo ya mchezaji bora wa msimu ikienda kwake pindi ligi itakapokuwa imemalizika

Mo Salah endelea kuishi katika miguu ya Ruud Van Nistelrooy

Sambaza....