Sambaza....

Wapwa,Wananchi leo wanaanza kampeni yao kutetea ubingwa wao kama si kuulinda watakapoanza mchezo wao wakwanza dhidi ya KMC Fc.

Msimu uliomalizika wao ndiyo mabingwa wakimaliza na alama 78 iliyotokana na ushindi katika michezo 25 sare 3 na kupoteza 2.

 

Wanaanza na KMC “Wanakinondoni” ambao msimu uliopita hawakufanya vyema hadi majaaliwa yao yakaamriwa kwa michezo ya “Play Off”.

Licha ya KMC kutokupata ushindi mara kwa mara dhidi ya Yanga kuna msimu pia walishinda wao wakazawadiwa kitita na aliyekuwa mkuu wa mkoa Dar-es -Salaam nyakati hizo Mh Paul Makonda.

Lakini kiukweli ‘Wananchi’ ndiyo wamekuwa wanapata matokeo zaidi wakutanapo.

Sasa basi kwa ule muonekano wa KMC kule Namungo katika mchezo wao wa kwanza itoshe kusema wana ujumbe tofauti msimu huu.

Kocha kijana Moalin inaonekana kukisuka kikosi vizuri muunganiko wa uchezaji unaonekana, wakitengeneza nafasi za maana na uwezo wa kufunga pia.

Hivyo basi mechi haitakuwa nyepesi au ya upande moja licha ya ukweli kuwa Yanga ni bora kuliko KMC.

Max Nzengeli.

Yanga iliyoongezewa nguvu kutoka kwenye kikosi cha msimu uliopiga cha Nabi inaonekana kuwa hatari.  Maingizo ya Yao, Nzengeli Pacome na wengine unagundua kuwa wanauhitaji wa kubakiza kombe tena msimu huu.

“Yote kwa yote nisema awike asiwike kutakucha”

Sambaza....