Sambaza....

Mshambuliaji wa Yanga sc, raia wa Zambia Obrey Cholla Chirwa ataukosa mchezo wa kwanza dhidi ya Woloyta Dicha kufuatia kuwa adhabu ya kadi mbili za njano alizopata katika michezo dhidi ya Township Rollers ya Botswana, huku habari njema ni kurejea kwa mshambuliaji Donald Ngoma.

Ngona aliyeanza mazoezi na kikosi hicho kwa takribani majuma mawili, baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha anapewa nafasi kubwa ya kuongoza safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa Tanzania.

Yanga inataraji kujitupa uwanjani kuwakaribisha Waloyta Dicha siku ya Jumamosi ijayo Aprili 7,2018 kunako uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumzia mchezo huo, meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kikosi chao kipo kwenye maandalizi ya mchezo huo na mshambuliaji Donald Ngoma ameonesha yuko fit kwa ajili ya mchezo huo.

“Kikosi kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo huo ambao tunahitaji kushinda”

Chirwa

“Kuhusu Ngoma ameonekana yuko fiti tangu alipoanza mazoezi na inawezekana akacheza endapo mwalimu akiamua kumtumia katika mchezo huo”.

Pamoja na Chirwa Yanga itawakosa Kelvin Patrick Yondan “Cotton”, Said Juma ” Makapu” na kiungo tegemezi kwa sasa kikosini Papy Kabamba Tshitshimbi, ambao pia wanatumikia adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano

Kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la soka Afirka (CAF) mchezaji hukosa mchezo mmoja endapo atafikisha idadi ya kuwa na kadi mbili za njano.

Sambaza....