Sambaza....

Taarifa zinaeleza kuwa matajiri wa Azam FC, wamemalizana na aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Donald Dombo Ngoma kwa kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja

Mwanzoni mwa juma lililopita ililipotiwa kuwa, Yanga imesitisha mkataba wa mshambuliaji huyo kutokana na kuwa majeruhi wa muda mrefu hali iliyopelekea kushindwa kupata huduma ya mchezaji huyo

Azam FC, italazimika kumfanyia matibabu mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe aliyekosekana uwanjani kwa takribani msimu mzima wa 2017/2018

Uongozi wa Azam FC, umekuwa ukikanusha kuhusiana na kumsajiri Ngoma lakini tetesi zinaeleza kuwa wamemalizana na mchezaji huyo

Donald Ngoma, alijiunga na Yanga SC akitokea FC Platinum ya Zimbabwe na kuiwezesha kutetea ubingwa kwa misimu miwili huku wakiunda safu kali ya ushambuliaji na Amis Tambwe

Itakumbukwa kuwa, Donald Ngoma, alipokuwa Yanga aliwahi kuwa chini ya Kocha Hans Van Der Pluijm ambaye pia anaelezwa kujiunga na Azam FC, hivyo wawili hao huenda wakakutana Chamazi.

Sambaza....