Sambaza....

Kumekuwa na maneno mengi sana mitandaoni kila mtu akionesha ufundi wake wa kulaumu iwe kwa makusudi ama kwa kutoelewa vizuri taarifa iliyotolewa juu ya michezo ya ndondo kufanyika kwa kibali

Wapo wanajaribu kuipotosha jamii…..lakini pia wapo wanaojaribu kuipa elimu jamii kuhusiana na taarifa hiyo iliyotolewa na Tff

Tff kimekuwa chombo cha kila mtu kujifunzia kulaumu, maneno yamekuwa mengi kana kwamba michezo hiyo imezuiliwa kabisa kufanyika nchini

Watu wanashindwa kuelewa kuwa Tff ndio chombo kinachotakiwa kuratibu na kusimamia mchezo wa soka nchini….hawa ndio Baba wenye dhamana ya kulea vilabu, vyama, viongozi wa ngazi zote kwenye mchezo huo pendwa nchini

Hivyo ni wajibu wao kuwa kila mashindano yatakayofanyika nchini kupata usimamizi wa kutosha kutoka Tff kwa kushirikiana na wanachama wake ambao ni vyama vya mikoa/ wilaya hii ni kwa faida kubwa ya mpira wa taifa hili

Ni wazi tu kuwa Tff katika hili bado wamesimama kwenye weledi na nia njema kwenye mpira wa Tanzania, na kwa kuzingatia masuala mbalimbali ya kikanuni katika mashindano husika ambayo ni lazima yafuate misingi sahihi ya Fifa na Tff

Tuache lawama zisizo na msingi hata kwenye masuala yenye ukweli tena yenye malengo ya kuleta maendeleo chanya katika mpira wetu…….tusijisahaulishe kuwa Tff ndio wanaobeba dhamana ya kuhakikisha mpira unachezwa kwa kufuata misingi ya kanuni na Tff ndio chombo kinachitakiwa kutoa baraka zake pale uwekezaji unapotakiwa kufanyika katika mashindano husika

Wakati umefika sasa wadau kwa kushirikiana na vyama husika kuiunga mkono Tff katika kutafuta mwarobaini wa mpira wetu na sio kuendekeza lawama kwenye kila jambo lifanywalo na chombo hiki….nieleweke tu kuwa sipingi kukosoa lakini tukosoe kwa jambo linalostahili, katika hili la vibali Tff wapo sahihi

Pongezi Rais Karia hili umeliona muda muafaka.

Sambaza....